RONALDO AIKAMATA REKODI YA RAUL ULAYA, AMKARIBIA MESSI REAL IKIUA 4-0
MWANASOKA bora wa dunia, Cristiano Ronaldo amefikia rekodi ya mabao ya mchezaji mwenzake wa zamani wa Real Madrid, Raul usiku huu baada ya kuifungia timu hiyo katika ushindi wa 4-0 dhidi ya RFC Ludogorets Razgrad.
Mshambuliaji huyo wa Ureno sasa anafikisha mabao 72 katika Ligi ya Mabingwa Ulaya na kubaki anazidiwa mawili tu na hasimu wake mkubwa, Lionel Messi wa Barcelona anayeongoza kwa sasa.
Ronaldo alifunga bao la kwanza Uwanja wa Bernabeu dakika ya 20 kwa penalti, kabla ya Gareth Bale kufunga la pili dakika ya 38, na wachezaji waliotokea benchi Alvaro Arbeloa kufunga la tatu dakika ya 80 na Alvaro Medran la nne dakika ya 88.
Ludogorets iliyopoteza mchezaji wake, Marcelonho aliyeonyeshwa kadi nyekundu dakika ya 19, inaaga michuano hiyo.
Kikosi cha Real Madrid kilikuwa: Navas, Arbeloa, Varane, Nacho, Coentrao/Marcelo dk60, Illarramendi, Kroos/Jese dk60, Isco, Bale/Medran dk83, Ronaldo na Hernandez
Ludogorets; Stoyanov; Junior Caicara, Terziev, Moti, Minev, Dyakov, Espinho/Anicet dk63, Aleksandrov/Wanderson dk61, Marcelinho, Misidjan/Azevedo Junior dk72 na Abalo.
Real Madrid stand-in captain Ronaldo wheels away in celebration after scoring past Ludogorets goalkeeper Vladislav Stoyanov@bin zubery
0 comments:
Post a Comment