PHIRI ASEMA CANNAVARO, YONDANI NDIYO KIZINGITI KIKUBWA KWA SIMBA
Wakati homa ya pambano la watani wa jadi kati ya Simba na Yanga ikizidi kupanda, Kocha Mkuu wa Simba, Mzambia, Patrick Phiri, ameweka wazi kuwa anawaogopa mabeki wa kati wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ na Kelvin Yondani tu.
Simba na Yanga zinatarajia kushuka dimbani wikiendi hii katika Uwanja wa Taifa kwenye mchezo wa bonanza la Nani Mtani Jembe 2.
Phiri alisema kikosi cha Yanga kina wachezaji wazuri wanaotoa changamoto lakini safu ya mabeki ya timu hiyo ambayo inaundwa na mabeki visiki, Cannavaro na Yondani ndiyo wanampa presha.
“Mpaka sasa nina hofu na mabeki wa kati wa Yanga, Cannavaro na Yondani tu kutokana na uwezo mkubwa walionao wa kuweza kucheza michezo mikubwa kama hii, pia wanaweza kuhimili mikikimikiki ya washambuliaji hatari.
“Na kama sitawapa mbinu za ziada washambuliaji wangu, tunaweza tusipate ushindi katika mchezo huo ambao ni muhimu kwa upande wetu,” alisema Phiri.
0 comments:
Post a Comment