PENZI LA WASTARA NA BONDI KIZUNGU-MKUTI

PENZI LA WASTARA NA BONDI KIZUNGU-MKUTI BAADA ya wiki iliyopita msanii wa filamu Bongo, Wastara Juma kuripotiwa kwenye moja ya magazeti pendwa kuwa hana uhusiano na mtu yeyote ndani ya Bongo Muvi na yupo mbioni kumuanika mrithi wa Sajuki mengi yameendelea kuibuka. Akizungumza na Uwazi, mpenzi wa Wastara anayetambulika kwa jina la Bondi Bin Salim alidai kuwa yupo kwenye mchakato wa mwisho wa kutoa mahari kwa ndugu wa msanii huyo kiasi cha shilingi milioni 5 pamoja na pete za dhahabu ili aweze kuwa na Wastara. Alisema kuwa maamuzi ya kutoa posa yamekuja baada ya kuona kila mmoja anaweza kuishi na mwingine kwani wameshasomana kwa muda mrefu. “Najua si jambo la watu kuhoji sana kwa sababu ndoa ipo na kila mtu atafanya hivyo, nina hela ya mahari tayari na siku ikipangwa ya kutoa tutafanya hivyo lakini ninachowaza sasa ni kuona nafanya vipi ili harusi yangu iwe ya kipekee na zoezi hili tutalifanya mwakani,” alisema
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: