ONE DAY YES sehemu ya 9

Jivunie kuwa mwana ludewa

ONE DAY YES sehemu ya 9














ONE DAY YES

Sehemu Ya 9

Mtunzi..... MoonBoy

Simu No. +255714419487 WhatsApp

Ilipoishia Jana ↓

"nami nashukuru sana kwa ukarimu wenu nami naamini mungu hatoniacha peke yangu"
Sasa nikiendelea kuwashukuru mara ghafla niliskia sauti ya broo
"kuma mayo bado hujaondoka tuu?"
Nilitoka mbio baada ya kuskia hivyo ila imeniuma roho kwa kutukaniwa mama yangu... ila sijali yote ni maisha tu... na naamini ipo siku na mimi nitatusua tu...... Daahh nilikua nipo hapo getini nikiendelea kufikiri pakwenda..
Niliangalia tu juu ya mbigu na kuongea neno moja tu
"ONE DAY YES"

ENDELEAAAA



Nilikua najifariji kwa maneno niliokua nikiongea mwenyewe kwani wakati huo nilikua nina hasira na maumivu ya mwili. Kwa kufukuzwa na kaka yangu wa damu kabisa Kisa ni mwanamke? daahh siamini kabisa kama leo nipo nje ya nyumba ya kaka yangu tena tajiri mkubwa hapa jijini arusha.....

Basi nilipotoka pale nilizunguka nyuma ya nyumba hio ya broo. wakati huo ilikua ni mida ya saa 4 usiku afu kuna baridi kali huku mvua ikianza kunyesha, Niliingia kwenye nyumba moja ya jirani na hapo. nyumba hio ilikua haijaisha kujengwa hivyo nilivaa lile koti la mlinzi na kutandika boksi ndani ya nyumba hio ambapo kulikua na vinyesi vya watu na pia ilikua ni kama nyumba ya mambwa.. kwani ilikua haina hata madirisha ya chuma ( magrili ) yaani ilikua ni behewa tuuu..

Kiukweli usingizi hauji kabisa kwani ndani ni ndani na nje ni nje.. Nimelala na vinyesi karibu nimelala na madogi pembeni.. Yaani nilikua kama mnyama vile. Lakini mungu sii asumani siku hio ilikwisha na sasa ni asubuhi....

Niliamka asubuhi sana kama saa 11 hivi alfajiri, Nilianza kujikokota na magongo yangu huku nikipita katika moja ya njia ambazo hata sizijui kwakweli.... Nilipita mahari na kukutana na vijana fulani hivi
"we vp saa hizi unatoka wapi?"
"mmhh?"
"mmhh nini? sema unatoka wapi?"
"asee natoka kulala jamani"
"ok ni furu areef sasa Ebu changia kidogo tupate ata dawa kidogo"
"dawa gani tena? kwani na nyie mnaumwa?"
Walinishangaa huku wakikonyezana kihuni
"oyaaa we wa wapi wewe? ata dawa ujui? ebu toa ata jala kimtindo areef"
Mmhhh sasa kwa vile walivyo vaa nikajua tu hawa ni wauni na nikikaa vibaya kale kapesa nilichopewa na jamila na mlinzi wataichukua hawa..
"ebana jodaa unae sanda areef?"
Eee sasa kuskia sanda nikajua heee apa kifo changu kimefika. lakini sana sio sanda kama sanda.. bali ni kikaratasi fulani cha kuekea bangi... ila mimi nilikua sijui kua ndio kinaitwa hivyo..
"jamani sasa sanda za nini tena ndugu zanguni?"
"afu we boya acha kutuzingua wewe tutoa iyo chambi tusepe Ama nini jodaa?"
"ni yechu yechu areef Au kama vp mbust kichere azinduke uyo"
Sasa niliposkia kubust nikajua hapa visu vya tumbo vitaniusu. maana mijitu ya arusha kwa fujo ndio wenyewe....

Niliona hawa wanaitaji pesa na kwakua nilikua na shilingi elfu 40 niliopewa na wafanyakazi wa broo... nilijisachi ili niwape ata elfu tano. maana wakisema wanisachi watachukua zote. Nilipata elfu tano kisha nikawapa...
"vp mbona umetoa kwa kuesabu? au una zingine nini? ebu tuone"
"Asee sasa si nishaawapa hio wazee?"
"Heeeeeee unamfokea nani we boya? nakuuliza kimbarata unamkoromea nani?"
"niachieni bhana"
"vunga we chalii tutavunja huu mguu mwingine we boya"
"lakini asee nimewakosea nini ndugu zangu?"
Walianza kunisachi huku mmoja kanishika. ila sikua na uwezo wa kuleta fujo kwani sikua na nguvu ya aina yeyote ile maana mguu mbovu mkono wenyewe pia mbovu tena ndio kwanza hata kupona havina hata dalili. Basi nilitulia tu kama dudumizi na kuchomolewa pesa zote nilizokua nazo...
"jamani nipeni ata iyo elfu 10 moja tu. maana jana sijala kabisa wazee"
"nani mzee wewe? peleka usambaa kwenu uko"
"oya jodaa mtemee iyo ng'ora yake ( simu yake ) kwanza haiuziki hii mpe tu"
"chukua uchafu wako endelea kutumia"
"wazee ata kaki basi niachieni"
Daa niliambulia kupewa simu yangu tu maana haiuziki kabisa...

Jamaa waliondoka na pesa yangu yote. na wakati huo mtoto wa kiume sina mbele wala nyuma na wala sijui kazi nitapata wapi na hata kama nikipata kazi je? nitaifanyaje? maana mguu na mkono wake havina kazi kabisa.... Basi niliendelea zangu kuchechemea na kuelekea mahali ambapo hata sipajui kabisa... kwani hata stend yenyewe tu siijui. Niliondoka hapo mpaka nimekutana na lami

Nikicheki saa ilikua ni mida ya saa 1 kasoro asubuhi... Kiukweli nilikua ni mtu mwenye njaa sana hivyo sikuona haya wala aibu ya kuelekea dampo na kutafuta hata chochote cha kutia tumboni.... maana jana nilifukuzwa kabla ya chakula. afu ukizingatia vyakula vyenyewe ndio hivyo...

Nilianza kutafuta ata maskonzi yaliotupwa kwenye dampo hilo. Nilikua sina kifurushi chochote nilichokibeba hivyo nilikua nipo mimi na gongo langu moja. Nilianza rasmi kula vyakula vya dampo. watu walikua wakinisikitia sana kwasababu shida zangu mimi zilipitiliza kikomo. kwani nilikua naumwa na afu bado sijapona afu bado hata usafi sina...

Sasa yapata wiki moja toka nifukuzwe na ndugu yangu.
Staili ya kula dampo na kulala dampo nilishaizoea maana sikua na pakula wala pakulala. na ulema wangu upo pale pale....

Siku ya leo dampo halikua na chakula hivyo nilianza kutembelea madampo yote makubwa makubwa na kukosa chakula kabisa.... Sasa nitafanyaje? maana hata kazi nashindwa kuomba maana sintoweza kufanya kazi kutokana na ukilema nilionao... Niliingia kwenye hotel ndogo ndogo na kuanza kuchangua madude ya kuekea vyakula vibovu... ambavyo kwangu naviona kama almasi vile. nilikutana na makapurwa wenzangu na kuungana nao na kuwa kitu kimoja.... Lakini mbaya zaidi wenzangu walikua ni waizi wa kupindukia. kwani wanajulikana hapo mjini kwa uizi.

WADUDU WA DAMPO ndio jina lao wanalotumia kujiita... Nilianza kujiunga nao rasmi kwakua wenzangu wanazijua sehemu zenye vyakula hivyo nami sikutaka kuwaacha wafanye yao. Walianza kunipa masharti yao na kuniambia kua
"sikia we mtu... Afu we ni msambaa Ee?"
"ndio"
"Aahahahahahaha duuu"
Walicheka kwa wote huku wakiangaliana.. . sasa nikajiuliza kua watu kama hawa wenye shida ya kupindikia nao wanafurahia kama mtu na pesa zake... Nami niliona haina haja ya kufikiria sana kuusu maisha....
"sikia we chaliii... ivi utaweza kazi wewe?"
"aaahh broo nitaweza"
"hahahahahahah uuu sasa taweza kukimbia wewe?"
"lakini nikipona nitaweza"
"sasa we pona kwanza afu ungana na sisi. maana sisi kazi zetu ni kukimbia muda wote. nadhani utakua umenielewa"
"sawa ila kwani hio kazi yenu haina seksheni zingine tofauti na hio?"
Mara mmoja akatoa wazo fulani
"ooiiii dadu?"
"sema totoo?"
"mimi nina wazo juu ya hilo"
"lete wazo"
"unaonaje huyu chalii akawa MR MAP?"
"yes safi sana totoo coz umetoa wazo zuri sana"
Niliuliza hio map ni nini
"wazee hio map ni kazi gani hio?"
Totoo ndio alinijibu kwa ufasaha tena bila kunificha kitu chochote
"sikiliza bhana naniii nani vile ulisema?"
"rashidi"
"ok sikiliza bhana rashidi... sisi kazi zetu ni uizi tu, tena uizi wetu hauchagui muda... yaani sisi tukiona pesa mahali hua hatuogpi kitu, hata kama askari wapo...hivyo ukiambiwa uwe mr map... basi ujue tumekuchagua uwe unatuangalizia muonekano wa pesa... mfano tukikutuma katika jongo fulani basi kazi yako wewe ni kuangalia njia za kutoke na njia za kuingilia.... yaani kwa kifupi utakua mchora ramani wetu maana wewe huwezi kukimbia.. kwahio hicho ndio kitengo chako kuanzia sasa hivi"

Kabla sijakubali nilianza kukumbuka familia yangu huku machozi yakinitoka kwa fujo. Na kukumbuka mateso yote ya nyuma mpaka sasa daahhh bora nikubali tu
"poa nimekubali jamani nifanye kazi na nyie"
Basi na mimi nilianza kua miongoni mwa watu wabaya tena makapurwa ( wachafu ) wa kutupwa

Siku moja tulikua katika hotel moja hivi ndogo ndogo tukitafuta chakula cha mchana katika zile ndoo za kuekea uchafu ( dastbin ) Tukiwa tunagombea makoko ya pilau.... Sasa mara kulitokea gari moja kali na kushuka mtu mmoja mwenye pesa zake. Na alifika hapo kwa kuja kumuona mtu.. maana alikua kama anaangaza angaza macho.. Alirudi kwenye gari na sikujua alichokifanya pale
"oyaaa chidi? nafasi yako ihusike pale"
"nafasi gani tena?"
"chora map tuanze kazi babaaa"
"daaahhh wezee kweupe ivi wazee?"
"sisi tulishakuambia kua hatuchaguagi muda"
"lakini wazee mbona mzee wa watu hana hata shida yule muislamu wa watu"
"hizo huruma za kisenge senge sisi ndio hatuzitaki sawa? tushaibia hadi mama zetu sembuse yeye??"
"oyaaa chaliii soma ramani chapu tuanze kazi"
"ok poa nipeni muongozo basi"
"nenda pale karibu yake msalimie afu muombe hela kama vile omba omba Akupe asikupe sisi tujulishe kama mkwanja upo tuvamie chapu"
"daah poa ngoja nijaribu"
"sio ujaribu..sisi hatuna hizo mambo za kujaribu"
"poa"
"na ukitusalitiii utajuata kuzawa duniani"
"acheni mkwara basiii"
"we nenda kafanye kazi bhana chalii"

Basi mtoto wa kiume kwa mara ya kwanza ndio naianza kazi ya uizi.... Sikusita kumsogerea yule mzee na kumsalimia.
"shkamoo mzee?"
"marahaba ujambo? Khaaa vp kijana mbona una vidonda kila mahari karibia mwili mzima?"
"daahh mzee wangu we acha tu ni maisha mzee"
"ok haya ulikua unasemaje?"
"mzeee? haki ya mungu vile mzee mi sijala toka jana mzee wangu.. sasa naomba uniseidie angalao hata senti nikapate hata skonzi kavu tu"
Nilikua nalia machozi ya uongo na kweli huku nikimuangalia kwa umakini sana huyu mzee...
Sasa ghafla mzee alitoa kitita cha pesa na kuanza kuhesabu moja baada ya nyingine.... Na kunipa pesa isiopungua elfu 50 tena ni mpyaaaaaa..........
Nilishindwa kuamini macho yangu.. maana hua naambiwa matajiri hua hawaseidiagi watu...
"saa nyingine unapomuomba mtu pesa usijaribu kumtaja mungu kabisa. maana wengine hatumuamini mungu sisi.. sawa?? kwahio hizo haki ya mungu zako ni huko huko unapoishi ila sio kumtajia mtu haki ya mungu... umenielewa?"
"ndio mzee asante sana na mungu akuja oooo samahani mzee kwa kusema mungu"
"najua sio kosa lako kijana"
Sasa mtoto wa kiume nilisahau kazi ilionileta hapo... mpaka wenzangu wakanishtua kwa mbaliii
"oyaaa unauweka sana chalii"
Nilitikisa kidole cha mwisho kuashiria "ngojeni kwanza" Sasa mzee alianza kuniuliza maswali
"umefanya nini mpaka umevunjika miguu mikonoo hebu ona sasa mabendeji yenyewe yamechafukaa ni nini kilikukuta kijana?"
"mzee ni maisha tu.. kwani nilipata ajali mzee"
Sasa kuangalia ndani ya gari niliona brifkesi iliofunuliwa. afu imejaa wekundu wekundu tupuuu... Duuuu nilipepesa macho kinafki na kujifanya sikuziona zile pesa...
"pole sana kijana wangu... pole sana. ila nahitaji nikupeleke hospitalini kijana"
Mara wale jamaa wakaanza kuja bila kuwapa ruksa ya kuja.....
Sasa nikajiuliza kua nimuambie kua watu hao wanaokuja sio wazuri au nisimuambie?? maana mzee keshaonesha kuniseidia kunipeleka hospitalini.... Nilimuangalia yule mzee kisha nikawaangalia na hawa WADUDU WA DAMPO wanavyokuja huku wakiwa wameshika visu..... na walisema nikiwasaliti kitu watanifanya sitokaa kusahau hadi kufa

Je? Nifanyeje hapo? Nipeni ushauri..
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: