ONE DAY YES sehemu ya 2

Jivunie kuwa mwana ludewa














ONE DAY YES

Sehemu Ya 2

Ilipoishia Jana ↓

Nilifika hadi mwisho wa lile korongo... yaani nikipiga hatua tu basi tena na sitokua mimi tena...
Sasa nilipofika hapo nilishindwa kujua pa kuelekea hivyo.. nilibaki tu nikiwa nimesimama pale

ghafla Kulidondoka jani la mti lakini sio jani kama jani... bali lilikua na ujumbe fulani..
Nililiokota na kulifungua kwa haraka
Heeeeeee nilishangaa kilichoandikwa humo kwenye hicho kijani
Eti kimeandikwa hivi
"usi.................

ENDELEAA……↓



Nilikua naogopa hata kufungua ile barua ya majani.. ila nilijikaza tu kiume huku nikittetemeka vibaya

Niliifungua ile barua na kuanza kuisoma.....
Heeeeeee nilishangaa kilichoandikwa humo kwenye hicho kijani
Eti kimeandikwa hivi
"usiende mjini"

Kiliandikwa hivyo tu basi. na hapo hapo kikanipotea kile kijani chenye ujumbe. Nilishidwa kuelewa kua ni nani kaniambia hivyo.... sijakaa vizuri mara kijani kingine kilikuja..
Kikiwa kimeandikwa hivi
"usimuambie mtu"
Kisha kikapotea pale pale mkononi mwangu.... Mara nilivutwa na broo na kurushwa huko pembeni..
"aaaaa sasa si utaniumiza broo"
"acha majanga wewe.. ulitaka kujiua pale si ndio?"
"nijiue kwa mpango gani sasa?"
Ilikua naongea lakini sina raha kwa meseji zile nilizozisoma muda sii mrefu...
"haya sasa ulikua unataka kufanyaje pale?"
Mmhhh nakumbuka niliambiwa nisimuambie mtu
"aaaa hamna kituuu wala"
"si unaona shem? mi nilikuambia ana masihara sana huyu mmeo"
Basi tuliamua kuondoka zetu...
lakini cha ajabu na cha kushangaza ule mguu nilioumia ulikua hauna kidonda tena... yaani kama vile sikuumia vile
"broo mbona sina kidonda tena?"
"aaaa ebu twende bhana nimechoka na mambo yako"
Nilikua nasema kweli ila yeye anaona ni utani. ila ni kweli kile kidonda hakipo tena, yaani utafikiri sikua nacho vile
basi tulikua tunakaribia nyumbani kwetu... huku mke wangu na mke wa kaka wakiwa mbele kama kawaida yetu.....

Tulifika nyumbani na kila mtu akaingia geto kwake, kwa ajili ya kupumzika kidogo ila mimi akili yangu ilikua ikiwaza kwa ile meseji niliopewa kule korongoni, sasa najiuliza ni nani kanipa ile barua??
Nilijiuliza sana lakini bado sipati jibu, Basi nilipumzika pale kidogo Ila sikulala sana kwani nilishtuliwa na sauti ya mtoto akilia
"aaaaaa nini tena mama saidi?"
"jamani mtoto anasumbua"
Nilimuonea sana huruma mke wangu maana alikua akifanya kazi huku mtoto akimsumbua, hivyo nilichukua jukumu la kumchukua mtoto wangu na kutoka nae nje ili mama ake afanye kazi....

Nilipotoka nilielekea nyumba kubwa, yaani hapa nikisema nyumba kubwa ninamaanisha kwa wazazi kule, maana hapa nilikua geto,
Basi nilipofika nilimkuta broo na mama pale wakiongea yao, Nilikaa nami nisikilize mawili matatu ila zumuni langu ni kumgusia mama katika swala la kwenda mjini, Baada ya wao kumaliza maongez nami nikaanza na yakwangu......

"sasa mama?"
"nini mwanangu?"
"mimi nina wazo kidogo"
"wazo gani? hebu sema tulisikie"
Mmhhh nilikua nasita kuongea ila najua tu hatokubali kabisa yani, maana katika hii familia sisi ndio tunategemewa kwa kuilisha familia...
"mama mi nataka niende kwa broo"
"Eti unasemaje? kwa broo yupi huyo?"
"si kaka hatibu"
"yaani rashid mwanangu huna hata wazo lolote unalowaza kuhusu familia,..... sasa sisi tutamtegemea nani humu ndani Eee? toka baba yako alipo fariki dunia... mpaka leo hakuna mtu anaetulisha kama sio wewe na kaka yako? mimi sikubaliani kabisa na wazo lako"
"mamaa kama ni chochote mimi nitarusha mama niache nikajaribu na mjini napo"
"nakuambia sitaki"
"lakini mamaa hujanitendea haki kabisa"
Kiukweli nilimbembeleza mama angu lakini wapiiii yaani hataki kabisa, Tulijitahidi hata kuongea na broo ili alizike lakini pia wapi...

Niliondoka pale na kumpeleka mtoto kwa mama ake.. kisha nikaenda kwa bibi kuongea nae...
Nilifika kwa bibi kisha nikamtoa kama na buku 2 ya ugolo ili nimlainishe na yeye..
"sasa bibi?"
"umeshaanza mambo yako tena? haya unasemaje?"
"amna bibi wala sina tatizo lolote"
"wataka nini?"
"sasa?? nataka ukaniombee kwa mama pale"
"nikakuombee nini sasa?"
"bibi mi nataka nikajaribu maisha na kungine"
"kivp sasa mbona sikuelewi mjukuu wangu?"
"bibiiii mi nataka niende mjini kwa kaka hatibu"
"weee mtoto wewe? uende mjini na familia yako nani ataiangalia Eee? mimi mwenyewe nawategemea nyie wajukuu zangu mnanipa hata ya ugolo afu leo unasema waondoka? Aa hapana mi sikuruusu uende"
"bibi kama ni chochote nitatuma tu msijali"
"hata kaka yako alipoondoka mwaka 2002 mwezi wa 9 alisema hivyo hivyo lakini matokeo yake hatumuoni hadi leo"
"huyo ni yeye bibi.. naomba tu mnikubalie ombi langu bibi"
"heeeeeee sasa ndio unalia?"
Nilikua natoa machozi ya uongo na kweli ili ajue kweli nataka kuondoka kwenda mjini hivyo,
Bibi aliniangalia na kunihurumia sana, na kama unavyojua mapenzi ya bibi yalivyo. hua hapendi mjukuu wake aumie pasipo na sababu yeyote
"haya basiii niongeze ya ugolo hapa nikaongee nae"
Nilinyanyuka na kutoa buku mbili tena, kisha nikampa bibi ili akaongee na mtoto wake ambae ni mama angu....

Baada ya hapo bibi alichukua mkongojo wake na kuelekea kwa mama.... sasa nikaona bora niondoke hapa ili niyakute matokea ila sio niyasubirie

Nilitoka pale nyumbani kwa bibi na kuelekea mtaani.. mida hio ilikua ni mida ya saa 10:30 jioni Wanafunz walikua wakirudi mashuleni.. nikiangalia hivi hua natamani kua mwanafunzi. kwani kama sio ugumu wa maisha basi leo ningelikua nipo kidato cha 3 ila daah ndio hivyo sasa, Nimefaulu vizuri sana tena kwenye matoke yangu ya darasa la saba nilipata Grade B yaani ni kiwango kizuri kweli, lakini kwa bahati mbaya wazazi wangu walikosa pesa ya kunisomesha hivyo ilifikia mahari mpaka niliuza jina langu kwa mtu aliofeli mtihani.. ili tu nipate kiasi cha pesa kwa kuendeleza maisha....

"oyaaa rashidi? we rashidi?
Daaahh alikua ni rafiki yangu mmoja niliekua nikisoma nae shule ya msingi,
Hata hivyo sikutaka kuonana nae kwasabu ni aibu kwa upande wangu..
"vip rashidi? ulikua unaninyamazia au ni mawazo tu?"
"daaa josee? mimi hapa nilipo sijiskii tena kua mtoto au kijana mdogo, kwani tayari najihisi nimeshakua mdingi wa makamo kutokana na haya maisha yetu ya tanga"
"hapana chidi wala usikate tamaa kiivyo, mbona we bado ni mdogo sana? au unajihofia kua una mke na mtoto?"
"wala tu sio hivyo josee ila ni majukumu nilionayo mimi.. sidhani kama hata huyo mtu mzima atakua nayo kwakweli"
"chidiiii sio wewe tu mwenye maisha magumu tuu. tena bora hata wewe unaepata hata milo miwili kwa siku...ila kuna mwenzio hajui hata harufu ya chai.. kwa maisha yake yalivyo magumu"
"aaaa sawa nashkuru kwa ushauri wako.... ila nina mpango wa kubadiri upepo"
"umeona sasa??? kumbe una mawazo ya mbali. wakati kuna mwenzi hawazi hata kupanda baiskeli..eee? kuna mwenzio anaisikia mjini kwenye redio tu.. kuna mwenzio haisikii hata harufu ya mjini.... chidi rafiki yangu nakuomba sana USIKATE TAMAAA maana ipo siku na wewe UTATUSUA tuuu... vp kwani unaondoka lini?"
"aaahhh bado sijajua ila nilimuambia maza lakini naona hataki.. na nimeongea na bibi muda si mrefu.. ili akaingee nae. sasa sijui kama atakubali au vp?"
"Usijali chidi huyo lazma atakubali tuuu... ila utaenda na mkeo?"
"mmm hapana kwakweli ila nitamuita kama mambo yatakwenda sawa"
"mmhhh poa ila ukienda kua makini sana rafki yangu si unajua una familia?"
"usijali josee nitawakumbuka tuu"
Mara simu yangu iliita... niliitoa na kuangalia alikua ni mmoja wa maboss zetu wanaotupaga mashamba ya kulima.... niliipokea
"haloo mzee shkamoo?"
"marahaba kijana hujambo?"
"sijambo mzee wangu. vp una kazi?"
"Eee ila nilimpigia kaka yako juma hapatka vp?"
"aaaa labda sumu yake itakua imeisha chaji"
"ok sasa? kesho nendeni kwenye shamba yangu ya mkonge... mlimie vizuri kama trekta.. maana nataka kupanda mahindi pale afu ile mikonge mkisha ichimbua muiweke mahali moja sawa?"
"sawa mzee nimekuskia..ila sisi hatuujui mpaka wa shamba lako vp sasa si uje utuelekeze mipaka kwanza?"
"aaahh usijali mimi nipo mbali ila mama razaki atakuja kuwaelekeza"
"sawa mzee tunashkuru mzee wangu"
"sawa ila hakikisheni mnachimbua kama trekta sawa? na ikiwa sivyo siwapi pesa"
"usijali mzee yaani tutachimba kama mifereji ya maji mzee"
"heeeeeeee mifereji??? ivi unaakili wewe? mifereji kwani una una unaaa kama hutaki kazi useme nikuache ufe njaaa"
"basi mzee nisamee ni utani tuuu"
"haya msichelewe lakini?"
"sawa?"

Daaahh tulimaliza kuongea vizuri kisha simu ikakata
"umeona maisha haya josee? yaani unapewa kazi na mikwara juuu"
"sasa utafanyaje chidi? ila mi nakuaminia lazima utoboe (utoke kimaisha)"
"daahh poa bhana... sasa mi naomba nikuache uwahi nyumbani nami nikajue michakato mizima ya familia yangu, si unajua?"
"yaaaa poa basi mida"
"poa Asee jose"

Ilikua ni mida ya saa 12 kasoro jioni hata safari ya kuenda kitaa iliisha hivyo nikawa narudi taratibu nyumbani.... ila nilianza kupitia kwa bibi kwanza ili nione kafikia wapi.. Nilimkuta bibi anatupia tu ugoro Hivyo nikakaa pale na kumuuliza kuuhusu jambo nililomuachia
"bibi mbona unacheka?"
"niongezee kidogo mjukuu wangu"
"aaaa bibi si unajua hata mafuta ya taa sina?"
Bibi alitaka nimuongeze hela ya ugoro duuuu
"hayaaaa eee ndio wataka kulia?"
"eeee mana staki kukudanganya bibi yangu"
"haya nilikuambia hilo ni jambo dogo tu"
"Eeeh unasema? unamaanisha kakubali?"
"jiandae tu mjukuu wangu... ila usikose kunitumia ya ugolo"
"bibi? unasema kweli kakubali?"
"ndio we nenda ukamalizie tu"
Nilikurupuka pale hata bibi sikumuaga na kuenda kwa mama angu ili kujua kama ni kweli kakubali....
Nilimkuta mama angu analia ila sikujua analia nini
"mamaa? mamaa? mama nini tatizo?"
"mwanangu? nakulilia wewe tuu maana wewe ndio kiziwanda wangu wa mwisho.. sasa naogopa usije ukazami kama kaka yako"
"mamaaaa mi siwezi kufanya hivyo eee? naomba unyamaze mama angu sitowatupa kweli?"
"mwanangu chidi nakupa baraka zote ila usitusahau wazazi wako mkeo mwenye mtoto mdogo... usije ukadanganywa na mihadaiko ya dunia"
"usijali mama lazima niwakumbuke tuu"
"nakuombea mwanangu"

Daaahh nilifurahi sana kuskia hivyo kwani nilijua angekataaa.. nilitoka mbio na kuenda geto kwangu huku nikiwa na furaha ya hali ya juu
"mke wangu mke wanguuuuuu hahahahaha nimekubaliwaaaaa"
"nini wewe baba said?"
"aaaahh we acha tu.. yaani safari imewivaaa"
"safari? safari gani?"
"Oohhh shiti kumbe skukuambiaga?? ooo naomba unisamee mke wangu.. kwani nia yangu ni kuwaomba wazaz kwanza afu ndio nikuambie"
Heeee mara mke wangu akaanza kulia
"iiiiii iiiiii uuuuiiii yaani chidi unataka kunitorokaaa"
"hapana hapana batuli mimi sifanyi hivyo?"
"sasa kama sio ni nini? si tayari ushaaongea na wazazi wako sasa mshaelewana...ndio unakuja kuniambia mimi"
"noo mke wangu usilie basi"
"kwani tutaenda wote?"
"mmm hapana"
"umeona sasa unanitoroka chidi"
"mke wanguuuuuu naomba utoe hilo wazooo kabisaa"
"chidi chidi chidi tumetoka mbali afu leo hii unanitoroka? kumbuka nimeacha shule kwa ajili yako chidi"
Nilijikuta nami naanza kulia tuuu kwa uchungu wa maneno yake Nilishindwa cha kuongea juu ya hilo kwani hata mimi huruma ya kumuacha mke wangu ilinijia ghafla tuuu

Basi kwa pale hatukuelewana kabisa maana kila mtu alikua ana ghazabu zake...
Alipika chochote tukala kisha tukalala zetu.... Siku hio nilikua na hamu ya naniii duuu maana toka mke wangu ajifungue mpaka leo ni miezi 6 sijawahi kugusa mzigo wa mke wangu tena...
Nilijaribu kumuamsha ili kama atakubali
"mama saidi, we mama saidi?"
"mmhhh?"
"vp sasa?"
"vp kuusu nini?"
Sikusema kitu bali nilianza kumpapasa mapaja na kushika kiuno chake, huku nikimtekenya tekenya kimahaba
"bwana chidi bado mtoto ni mdogo wewe"
"aaaa mke wangu usifanye hivyo"
"sitaki bwana niachie.. tutamuumiza mtoto"
"aaaa msogeze hukoo ili tusimguse"
"sio hivyo mume wangu... tukifanya mapenzi tukiwa na mtoto mdogo sio vizuri"
"we muongo wewe... kwan ni nani kakuambia?"
"si mama angu?"
"mmhh we sema hutaki tuuu"

"haya basi njoo ila ujue mtoto wako hatotembea maisha yake yote"
"Eti nini? weeed ninavyompenda mwanangu hivyo..tena natamani atembee hata leo hii afu unaniambia hatotembea??? kama ni hivyo basi staki we lala zako tu"
"aaa kama wataka chukua ila kasaid chako katabaki chini maisha yote"
"sitaki bwana nishagaili.... ila nina hamu hio mke wangu.. kwani we huna?"
"ninayo tele"
"sasa mbona hata huniombi"
"kwani si ninajua madhara"
"mmhhh haya... ila nina hamu hio duu"
"utajiju mi mwenzio najikandaga na maji ya moto"
"haaaaaaa sasa si bora wewe mimi je?"
"sikia mume wangu... nakuruusu chepuka mara moja tu ila usizoee"
"aaacha utani batuli"
"kweli ila utumie kinga"
"uuuuuuwiiiiii safi sana tuturururu"
"sasa unaenda wapi?"
"si naeda kwenye mdumange huko husikii?"
"sijakuambia uchepuke leo"
"aaaaaaa mboa unabadirika tena mke wangu?"
"kesho ila leo laza miguu yako hapa"
"Eeee yashaakua hayo tena?"
"lala bwana kwani hadi kesho utakufa?"
"haya basi mke wangu.... sasa mke wangu?"
"nini tena?"
"umekubali kuusu safari?"
"chidi chidi chidi usinitibue bwana"
"mmhh basi yaishe"

Sasa mtoto wa kiume nilijiwa na mawazo juu ya yule mtu alienitumia ule ujumbe kule korongoni.. nilikua nina mawazo sana. kwani hata usingizi ulikua hauji kabisa yani.. Niliwaza sana kuusu yule mtu. maana smjui ni jinsia gani wala ni nani...
"we baba saidi hujalala tu?"
"we mbona hujalala?"
"mi nawaza ukiondoka je nitabaki na nani?"
"usijali mke wangu... nitakua nakutumia chochote"
"sasa utanitumiaje?"
"nitakuachia simu yangu usijali"
"mmhhh ila baba saidi naomba usinisahau mimi na mwanao"
"hakuna watu ninaowapenda sana kama nyie wewe na mtoto wetu"
"sawa nimekubali"
"saaafi sana mke wangu... haya ndio mafanikio sasa"

Sasa tukiwa nampongeza kwa kunikubalia kusafiri.. nilikua namyonya denda... lakini ghafla bin vuu kibatali kilizimika na hakukua na upepo wowote ule
"mbona umezima taa mama said?"
"mi sijazima jamani.."
"hebu lete kiberiti..maana hakutakiwi kuwe na giza kwa ajili ya mtoto"
"nilishika kiberiti lakini cha ajabu mikono yangu ilikua ikitetemeka vibaya mno.. kiaskwamba hata kuwasha kiberiti nilikua siwezi....
"washa basi mume wangu"
"mama said mbona sielewi"
"huelewi nini?"
Mara kulitokea mwanga mkaliii pembezoni mwa ukuta kisha ikarusha barua nyeupeeee ilioambatana na mwanga mkali sana
niliachia kiberi na kuipokea ile barua ilioandikwa hivi

"bado husikii tu? Nimeshakwambia usiende mjini"

Kisha ilitoweka mikononi mwangu ile barua kisha kukawa giza
"mama saidi umeona nini?"
Nilimuuliza mke wangu kama kaona ule mwanga
"sijaona kitu mbona"
"Eeee mungu wangu hebu muangalie mtoto wetu yupo?"
"sasa ataenda wapi? Heeeeeee mume wangu mtoto simuoni"

Usikose kuifatilia sehemu ya 3 hapo kesho mida kama hiii

bonyeza LIKE ili iendeleeee kesho
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: