Jivunie kuwa mwana ludewa
Na MatukiodaimaBlog MBUNGE wa jimbo la Kalenga Bw Godfrey Mgimwa amewapongeza wananchi wa jimbo hilo kwa kuonyesha imani kwake na chama cha mapinduzi (CCM) baada ya wananchi hao kukiwezesha chama tawala kushinda kwa kishindo kwa kupata vijiji 73 kati ya vijijini 74 huku chama cha Demokrasia na maendeleo (Chadema)kikiambulia kijiji kimoja pekee.
Mbunge Mgimwa katika salam zake za pongezi kwa wananchi wa jimbo la Kalenga leo alisema kuwa amefarijika zaidi na imani kubwa ambayo wananchi wa jimbo hilo wameonyesha kwake na CCM kwa ujumla .
“Imani kubwa sana wananchi wa jimbo la Kalenga mmeweza kunionyesha kama mbunge wenu pia ni wazi kazi inayofanywa na serikali ya CCM kwa wananchi wa jimbo hilo imeendelea kuwajengea imani zaidi wananchi wangu”
Mwenyekiti wa CCM mkoa Jesca Msambatavangu kulia katibu wa CM wilaya Amina Himbo na wapili kushoto ni mbunge Mgimwa na viongozi wengine katika picha ya pamoja .
…………………………………………………………………………………….
Pia Mbunge Mgimwa aliwapongeza viongozi wa jumuiya zote za CCM mkoa , wilaya ya Iringa vijijini kwa ushirikiano mzuri wa kunadi sera za chama wakati wa kampeni za chaguzi za serikali za mitaa na kuwa umoja ambao viongozi hao wa wilaya na kata wakiwemo madiwani ni moja ya sababu kuwa ya ushindi wa CCM dhidi ya Chadema.
Hivyo alisema kwa nafasi yake ya ubunge katika jimbo hilo la Kalenga ni kuona ahadi mbali mbali alizozipokea kutoka kwa mbunge aliyetangulia mbele za haki Dr Wiliam Mgimwa zinatekelezwa kama alivyopata kuwaahidi wakati wa kampeni za uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo hilo mapema mwaka huu.
Alisema toka amechaguliwa na kuapishwa kuwa mbunge wa jimbo hilo la Kalenga amefanikiwa kutekeleza ahadi mbali mbali ikiwemo ya maji ,umeme katika kata mbali mbali ikiwemo ya Mgama na nyingine pia kuchangia miradi mbali mbali ya kimaendeleo inayoendeshwa na wananchi pamoja na kuanzisha vikundi vya Vicoba kwa wananchi wa maeneo mbali mbali ya jimbo hilo.
Mwenyekiti wa Chadema Taifa Bw Mbowe akimnadi mgombea ubunge wa Chadema jimbo la kalenga Grace Tendega aliyeshindwa na Mgimwa……………………………………………………………………………………………… Mbunge Mgimwa alisema kuwa katika uchaguzi huo wa serikali za mitaa kata ya Ifunda ambayo ndio ilikuwa na nguvu kubwa ya upinzani CCM ilipata kushinda vijiji vyote 6 na kupata vitongoji 31 huku Chadema wakipata kitongoji kimoja pekee,kata ya Lyamungungwe vijiji vyote 6 na vitongoji 36 vilichukuliwa na CCM ,kata ya Magulilwa kati ya vijiji 6 CCM ilishinda vijiji 5 na Chadema kimoja wakati vitongoji 42 vilichukuliwa na CCM na Chadema kupata vitongoji 4,kata ya Luhota yenye vijiji 5 na vitongoji 46 CCM ilishinda vyote ,kata ya Mseke yenye vijiji 4 na vitongoji 25 vyote vilichukuliwa na CCM na Kata ya Ulanda vijiji vyote 6 vilichukuliwa na CCM wakati vitongoji 33 CCM ilishinda na Chadema kupata
kimoja pekee.
Kwa upande wa kata ya Maboga yenye vijiji 3 na vitongoji 25 vyote vilichukuliwa na CCM huku Chadema wakiachwa patupu ,kata ya KIhanga yenye vijiji 5 na vitongoji 27 vyote vilichukuliwa na CCM ,kata ya Mgama vijiji vyote 6 vilichukuliwa na CCM wakati vitongoji 45 vilichukuliwa na CCM na Chadema kupata vitongoji 2 ,kata ya Kiwere CCM ilishinda vijiji vyote 5 na vitongoji 20 dhidi ya kitongoji kimoja ambacho Chadema walipata kwa kata ya Masaka vijiji vyote vitatu vilichukuliwa na CCM wakati kitongoji 1 kilichukuliwa na Chadema na CCM kupata vitongoji 16
Kata ya Lumuli vijiji vyote 4 na vitongoji 22 vilichukuliwa na CCM wakati kata ya Kalenga vijiji vyote vitatu CCM na kati ya vitongoji 10 Chadema walipata kimoja pekee na CCM 9,kata ya Wasa vijiji 7 vyote vilichukuliwa na CCM na upande wa vitongoji CCM ilishinda vitongoji 4 na Chadema 3 na kata ya Nzihi yenye vijiji 6 na vitongoji 44 vyote vilichukuliwa na CCM .
Alisema pamoja na uchaguzi huo kuonekana kuwa mgumu zaidi katika baadhi ya majimbo nchini ila kwa upande wa Kalenga CCM imepata kushinda vijiji 73 kati ya 74 wakati vitongoji 445 vimechukuliwa na CCM na Chadema kuambulia vitongoji 9 pekee.
Katibu mkuu wa CCM Bw Kinana akimnadi Mgimwa (kulia) wakati wa kampeni jimboni Kalenga |

0 comments:
Post a Comment