NYOSSO WA MBEYA CITY, ATUMA SALAMA DAR ES SALAAM

Beki wa kati wa Mbeya City, Juma Said Nyosso ‘Baba Saidi’ amefunguka kuwa hawahofii washambuliaji wa Yanga, Amisi Tambwe, Kpah Sherman na Danny Mrwanda katika mchezo watakaokutana baada ya Yanga kutoka kwenye Kombe la Mapinduzi. Nyosso aliiongoza Mbeya City kuibuika na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Ndanda FC ya Mtwara, katika mchezo uliochezwa wikiendi iliyopita ikiwa ni ushindi wa pili tangu ligi ianze. Yanga na Mbeya City zitakutana katika Uwanja wa Sokoine Mbeya, katika mchezo wa raundi ya tisa wa Ligi Kuu Bara. Nyosso alifunguka kuwa hawahofii washambuliaji wa Yanga akiwemo Tambwe, kwa kuwa kazi yake ni kuhakikisha timu yake hiyo inashinda michezo yote iliyopo mbele yao. “Nashukuru Mungu kuona tumeanza vizuri, kwenye ligi kwa kushinda bao moja dhidi ya Ndanda na tayari nimeshaelewana na mabeki niliowakuta kwani lengo letu ni kuhakikisha tunapata ushindi katika kila mechi. “Tumejiandaa kwa ajili ya mechi zote za ligi na si Yanga pekee kwa kuwa lengo letu ni kuona timu inakuwa kileleni. “Kwa muda mfupi niliokaa na wachezaji wezangu tayari tumeshaelewana na nipo vizuri hata mechi dhidi ya Yanga hakika simhofii Tambwe wala mchezaji yeyote wenyewe waje tu wataona kazi,” alisema Nyosso.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: