Mtunisi aendelea kusota ndani baada ya kumpiga mkewe

Msanii wa filamu, Mtunisi aliyepandishwa mahakamani Jumatatu iliyopita kutokana na shtaka la kumshambulia mke wake, ameendelea kukaa ndani baada ya kukataliwa dhamana kufuatia mkewe kuwa kwenye hali mbaya. Akizungumza nasi, muigizaji mwenzake, Batulli amesema wanashindwa kuingilia suala hilo moja kwa moja kwa sababu limekaa kifamilia zaidi. “Tunafuatilia lakini unajua bahati mbaya kidogo tatizo lake limekaa kifamilia zaidi, yaani ni mke na mume. Kwahiyo mimi siwezi kuingilia sana kwa sababu at the end wale ni mke na mume wanatakiwa waheshimiane wenyewe. Wanadai mwanamke amepigwa na ameumia vibaya na bado yupo hospitali. Sasa kisheria nasikia hawawezi kumuachia mpaka mwanamke apate nafuu,”alisema Batuli. Hakimu wa wa mahakama hiyo ya mwanzo ya Manzese/Sinza aliahirisha kesi hiyo hadi Desemba 15 mwaka huu itakapotajwa tena.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: