HATARI: MAFUNDI WAKUTA MABOMU 8 WAKATI WAKIJENGA NYUMBA HUKO KIGOMA

Mafundi uashi wawili wamegundua mabomu manane ya kutupwa kwa mkono ambayo inasemekana yamekuwepo ardhini kwa Zaidi ya miaka 10 Kigoma kwenye Kijiji cha Mabamba walipokuwa wakichimba msingi wa nyumba ya Mganga wa Kituo cha Afya. Mafundi hao wamesema baada ya kubaini kuwepo kwa chuma ambacho hawakukitambua waliamua kutoa taarifa Polisi na Jeshi la Wananchi JWTZ, ambapo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma Jafari Mohamed amethibitisha kutoa kwa tukio hilo. Kamanda huyo amesema wanaendelea kuwahoji watu kadhaa ikiwemo Diwani wa wa Kata hiyo ambaye alikuwa anaimiliki nyumba hiyo kabla ya kuiuzia Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo, Mkuu wa Wilaya ya Kibondo Venance Mwamoto amesema huenda mabomu hayo yaliachwa na wapiganaji wa kutoka Burundi walipokuwa nchini kama Wakimbizi.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: