MTUHUMIWA WA WIZI NA MAUAJI WA MADEREVA WA BODABODA AJISALIMISHA POLISI... MADEREVA WAVAMIA KITUO
Baada ya kuona hili la kumpata Mtuhumiwa linashindikana bodaboda waliamua kuitana kila wanapopita ili kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa ili wachome moto nyumba yake.
Tukio hili limewashtua wakazi wengi waliokuwa hawajui na kuja eneo la Msalala road kuangalia kulikoni huku jeshi la polisi likihakikisha hali ya usalama inaendelea kuimarika.
Mtuhumiwa Juma Itibango alikuwa akifanya biashara katika soko la Mjini Geita, na kama haitoshi eneo lake la biashara lilivamiwa na kila mtu kuchukua alichoweza na hata baadhi ya wafanyabiashara walibebewa mali zao.
Hata hivyo waendesha bodaboda walilitaka jeshi la polisi kutopuuza matukio wanayoyapata kwani mara kadhaa wamekuwa wakiuwawa lakini wanadai hatua za haraka hazichukuliwi.
Mtuhumiwa Itibango jana asubui alionekana na bodaboda ambayo inadaiwa iliibiwa ndipo mwenye mali alimuona na kuwaita wenzake ili kujinusuru Juma alikimbia akiwa na abiria ambaye katika kukimbia walianguka na abiria kuumia.Waendesha Pikipiki mjini Geita wameizingira ofisi ya Polisi Mkoa baada ya mtu wanayemtuhumu kuhusika kwenye matukio ya wizi na mauaji ya waendesha bodaboda kukimbilia polisi kujisalimisha.
Waendesha bodaboda hao ambao wamekaa kwa muda nje ya ofisi hiyo wamefikia maamuzi ya kwenda nyumbani kwa mtuhumiwa ili wachome nyumba yake wakidai mtuhumiwa huyo amekuwa akikamatwa na kuachiwa.
0 comments:
Post a Comment