MOROGORO YAKUMBWA NA MAFURIKO LEO

Mvua kubwa zilizonyesha kwa muda mfupi mjini Morogoro zimesababisha mafuriko baadhi ya barabara kushindwa kupitika na maji kujaa katika baadhi ya maduka. Wakazi wa mji wa Morogoro wakizungumzia mafuriko hayo wamelalamikia miundombinu mibovu ya barabara kutokana na kuziba kwa mitaro ambapo wameitaka halmasauri ya mji wa Morogoro kuzibua mitaro hiyo huku baadhi ya wafanyabiashara wakilalamikia kupata hasara. Katika hatua nyingine mto Kikundi uliopo mjini Morogoro umepoteza uelekeo na kumwaga maji katika soko kuu la mji wa Morogoro na kusababisha maji kujaa katika maduka huku baadhi ya magari yakiingia kwenye mitaro na baadhi ya bodaboda zikiwa na abiria zime zama katika maji na kulazimika kuvutwa. Kaimu mkurugenzi wa manispaa ya Morogoro Phimlemon Magesa akizungumzia alalamiko hayo ya wananchi hao amesema manispaa wanajitahidi kufanya usafi lakini tatizo liko kwa wananchi wenyewe kutupa taka kwenye mitaro na kusabisha mitaro hiyo kuziba na maji kupoteza ueleko na kujaa katika makazi ya wananchi. via>> itv.co.tz
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: