MTIBWA SUGAR WATUA KYELA TAYARI KUWAVAA WAMALAWI, WAZAMBIA
Mtibwa Sugar imesili mjini Kyela tayari kwa ajili ya mechi zake za kirafiki kujiandaa na Ligi Kuu Bara.
Vinara wa Ligi Kuu Tanzania, Mtibwa Sugar, wanatarajia kucheza mechi za kirafiki dhidi ya timu kutoka katika nchi za Malawi na Zambia.
Kikosi hicho ambacho kimekuwa kwenye ‘fomu’ ya hali ya juu, ambapo Jumapili kiliinywesha Simba mabao 4-2 katika mchezo wa kirafiki, kinatarajia kuondoka leo Jumatano kwenda mkoani Ruvuma.
Kikiwa hapo kitacheza mechi tatu, ikiwemo dhidi ya Mbeya City kabla ya kuelekea Kyela ambako kitacheza mechi kadhaa na timu za wilayani hapo pamoja na zile za Zambia.
Ofisa habari wa kikosi hicho, Thobias Kifaru, alisema wameamua kwenda mikoa hiyo baada ya kuombwa na wadau wa soka.
“Tayari kila kitu tumeishapanga na kesho (leo) tunatarajia kuondoka kwenda Songea (mkoani Ruvuma) tutacheza mechi kama mbili, tatu ikiwemo dhidi ya Majimaji na Mbeya City, kisha tutaelekea Kyela (Mbeya) pia tutakuwa na mechi, lakini hapo kuna timu za Zambia zitakuja kucheza na sisi,” alisema Kifaru.
0 comments:
Post a Comment