MSICHANA AJIFUNGUA MTOTO MWENYEWE NA KUMTUPA KWENYE NDOO HUKO ARUSHA

Msichana mmoja mkazi wa mtaa wa Zaire Mkoani Arusha,amelazwa katika hospitali ya Mount Meru Arusha chini ya ulinzi mkali wa polisi baada ya kujizalisha mwenyewe kisha kumtumbukiza mtoto kwenye ndoo ya maji. Baba mwenye nyumba ambayo binti huyo alikua amepanga chumba cha kuishi,Ruben Mollel alisema msichana huyo alikua anajulikana kwa jina la Dada Pendo na kwamba maisha yake hayakua wazi. “Alipokuja kupanga hapa alidai yeye ni mwanafunzi,ila hivi karibuni alionekana kuwa mjamzito,hakuna kilichojulikana tena hadi jana ambapo nyumba hii ilizingirwa na wanakijiji ambao hatimaye waligundua kitoto kilichadhaniwa kuwa ni chake kikiwa kimezamishwa kichwa chini kwenye ndoo ya maji”alisema baba huyo mwenye nyumba. Taarifa za uwezekano wa kuwepo mtoto huyo ndani ya nyumba ya dada huyo ziliibuliwa na mpangaji mwenzake Mama Martha ambaye alidai kuwa alisikia sauti ya mtoto akilia usiku kucha na baadaye kutoweka majira ya asubuhi. Baada ya juhudi za kuchunguza walikuta kichanga hicho cha kiume kikiwa ndani ya ndoo na tayarikilikua kimefariki dunia huku mama yake akiwa katika hali mbaya kutokana na kujizalisha mwenyewe.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: