MSHAMBULIAJI DANNY MRWANDA AMWAGA WINO YANGA USIKU HUU

Mshambuliaji Danny Mrwanda amemwaga wino wa kuitumikia klabu ya Yanga ya jijini Dar es salaam kwa mkataba wa mwaka mmoja usiku huu. Yanga imewafanyia umafia watani zao wa jadi Simba,ambayo ilionyesha nia kubwa ya kumuhitaji Mrwanda ikiwa ni kwa hudi na uvumba na tayariilishatangaza nia yake hiyo ya kutaka kumsajili. Chanzo cha kuaminika kutoka ndani ya Klabu ya Yanga kinasema kuwa,Yanga imeamua kumsajili Mrwanda kuchukua nafasi ya Said Bahanuzi aliyetolewa kwa mkopo kwenda Polisi Morogoro wakati Jerry Tegete akiwa ni majeruhi,na mshambuliaji pekee wa ndani wanayemtegemea ni Hussein Javu.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: