MKURUGENZI MTENDAJI LUDEWA AKEMEA VITENDO VYA WATUMISHI WA UMMA KUJIHUSISHA NA KAMPENI ZA KISIASA
uchaguzi wa serikali za mitaa Viongzi wa vyama vya siasa wilayani ludewa mkoani njombe wametakiwa kuacha tabia ya uvunjifu wa amani na kutambua kuwa uchaguzi wa serikali za miataa si vita bali ni amani kwa kuchagua viongozi ambao wataleta maendeleo katika jamii.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi mtendaji halmashauri ya Wilaya ya Ludewa bw,William Waziri wakati akizungumza na mmiliki wa mtandao huu ofisini kwake na kuwa amefikia hatua ya kutoa kauli hiyo mara baada ya kutapa taarifa kuwa baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa wanachoma bendera na kuzishusha kiholela kitendo ambacho ni kinyume na sheria za uchaguzi huo.
Aidha amesema kuwa mchezo huo mbaya wa kuchoma bendera na kushusha bendera kiholela umejitokeza katika maeneo ya mlangali na mundindi wilayani hapa huku akisisitiza kuwa suala zima la uchaguzi wa serikali za mitaa halihusiani na uchomaji bendera wa bendera hizo.
Akizungumzia tabia ya baadhi ya watendaji wa vijiji na kata kujihusisha na suala la kampeni bw, waziri alisema kuwa mtumishi yeyote katika utumishi wa umma anaongozwa na sheria,kanuni na taratibu pamoja na maadili ya kazi hivyo anashangazwa na watendaji hao ambao wanajihusisha na kampeni kwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume na taratibu hizo.
Aidha amewataka watendaji hao kuacha tabia ya kuongozwa na hisia ya kujihusisha na masuala ya kisiasa kwani kufanya hivyo ni kukiuka kanuni na sheria zilizowekwa na kuwataka wananchi kushiriki katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika jumapili hii kwa lengo la kuwachagua viongozi wanaowataka huku akisema kwa mtendaji atakaye kiuka agizo hilo ajuekuwa atakuwa hana kazi kwa kufukuzwa kutokana na vitendo hivyo.
0 comments:
Post a Comment