MAABARA ZAKAMILIKA WILAYANI LUDEWA KATIKA MKOA WA NJOMBE
Desember 9 mwaka huu ilikuwa siku ya mwisho ya kukamilisha na kukabidhi maabara tatu kwa kila shule ya sekondari hapa nchini Tanzaniakama lilivyo tolewa agizo kutoka kwa Raisi wa Jamuhuri ya muungano wa Tanzania Mh, Jakaya Mrisho Kikwete agizo ambalo limetekelezwa kwa baadhi ya halmashauri hapa nchini kukamilisha kwa kiwango kinachoridhisha na baadhi ya halmashauri zimeonekana kuto fikia na kutekeleza agizo hilo.
Kwa upande wa halmashauri ya wilaya ya ludewa katika mkoa wa njombe haliimeonekana kuwa ya kuridhisha kutokana na baadhi yamaabara kukamilika kwa asilimia mia moja na baadhi ya maabarahizo zikiwa katika hatua ya mwisho ilikukamilika na kuanza kutumika.
Akizungumza na mtandao huu hivi karibuni mara alipokuwa ofisini kwake mkuu wa wilaya ya ludewa mkoani njombe Bw, Jumma Solomoni Madaha alisema kuwa mpaka sasa maabara zilizo kamilika kwakuanza kutumika ni 15 na ambazo zimekamilika lakini hazina samani za ndani ni maabara 14 na maabara 21 zimejengwa kilicho baki ni kupiga lipu na kuingiza vifaa kwaajiri ya kuanza kutumika na wanafunzi wa shule hizo, Huku akisema kuwa maabara ambayo haija jengwa kabisa kwa wilaya ya ludewa ni maabara moja tu ambayoipo katika shule ya sekondari ketewaka.
Hata hivyo mkuu huyo alieleza sababu iliyokwamisha ujenzi wa maabara hiyo moja kuwa ni uongozi wa vijiji na kata kutokana na shule ya sekondari ketewaka kuhudumiwa na kusimamiwa na kata mbili ambazo ni kata ya mkomang’ombe na kata ya iwela hivyo wananchi wa kata hizo wamekuwa wakivutana na kubishana juu ya ujenzi wa maabara katika shule hiyo.
Akizungumzia kukamilika kwa ujenzi wa maabara hizo bw, Madaha alisema kuwa kukamilika kwa ujenzi huo kumetegemea sana nguvu za wananchi hivyo kila kata ilijiwekea mpango wake ilikuweza kukamilisha kazi hii ya ujenzi.
“mfano ukienda katika shule ya sekondari manda ile shule inachangiwa na kata ya luhuhu ambayo haina sekondari na manda yenyewe ukija katika shule ya mchuchuma inachangiwa na kata ya masasi na kata ya lwilo kwahiyo ni mpango wa wananchi wenyewe hivyo hata mimi kama juma Madaha nimetoa mchango wangu katika shule ya sekondari chief kidulile iliyoko hapa ludewa mjini” Alisema mkuu huyo wa wilaya.
Hata hivyo aliongeza kuwa mpango wa uongozi wa wilaya ya ludewa ni kwamba wanafunzi watakapo fungua shule mwezi January 2015 maabara zote ziwe zimekamilika.
Mwishooo.
0 comments:
Post a Comment