MAREKANI YATUMA MANUWARI KUITAFUTA AIR ASIA

Wanamaji kutoka Marekani wamesema kuwa wanapeleka moja ya Manuwari ya kivita kutafuta ndege ya AirAsia iliyopotea tangu jumapili katika Bahari za Indonesia. Manuwari hiyo ijulikanayo kwa jina la USS Sampson inatarajiwa kufika leo katika eneo la Java Sea today ikiwa ni siku ya tatu tangua kuanza msako dhidi ya ndege hiyo. Idadi ya wataalamu wa kimataifa wanaoitafuta ndege hiyo imeongezeka ambapo kwa sasa nchi za Singapore, Malaysia ,Australia,Korea Kusini,Thailand na China wanashiriki katika kazi hiyo. Mkuu wa Operesheni ya uokoaji na utafutaji ndege hiyo Henry Bambang Soelistyo amesema kwa sasa kuna jumla ya Meli 30, ndege 15 na Helkopita katika eneo la tukio. Ndege hiyo ilipotea ilipokuwa ikisafiri kutoka Surabaya Indonesia kuelekea Singapore ikiwa na abiria 162.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: