i wish you happy chrismass and happy new year Kocha anayesifika kwa ukali wenye kuwajenga wachezaji, Hans van Der Pluijm. KOCHA anayesifika kwa ukali wenye kuwajenga wachezaji, Hans van Der Pluijm, jana aliwabwatukia mazoezini nyota wake, Mliberia, Kpah Sherman na Simon Msuva. Tukio hilo lilijiri jana katika mazoezi ya kikosi hicho yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Boko, Ununio wakijiandaa na mchezo wa kesho Jumapili wa ligi kuu dhidi ya mabingwa watetezi, Azam. Championi Jumamosi lilikuwa shuhuda wa tukio hilo, ambapo Pluijm alionekana kukerwa na nyota hao kushindwa kufuata maelekezo ya mbinu zake alizokuwa akiwapa hali iliyomfanya kung’aka kwa hasira. Msuva alikuwa akimkoroga kwa kushindwa kujipanga vema katika kutafuta mipira na kukaba, ambapo alisimamisha mazoezi mara kadhaa kabla ya kung’aka, hata hivyo Sherman baadaye alionekana kuharibu kutokana na kushindwa kuzitumia vema pasi za kutanguliziwa (penetration passes). Pia Mliberia huyo alikuwa akikosolewa juu ya kutumia vema nafasi za mwisho ambapo hata kocha msaidizi, Charles Mkwasa aliamua kumuelekeza nyota huyo.Lakini mbali na hilo, nyota huyo alionekana kuwa mwiba mkali kwa kupiga mashuti mazito golini wakati wa zoezi la kupiga faulo, ambapo alifunga moja na kugongesha mwamba na kupaisha mara mbili.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: