Baby Madaha: Napenda mapenzi yananipa starehe kuliko kitu chochote hapa duniani

MWANADADA asiyeishiwa matukio Bongo, Baby Madaha ameibuka na kutoa kali ya mwaka kwamba anapenda mapenzi kuliko kitu kingine chochote duniani. Akichezesha taya na paparazi wetu, Baby Madaha alisema ‘hobi’ yake ni mapenzi japokuwa anapenda muziki lakini haifikii jinsi anavyoyapenda mapenzi kwani yanampumzisha akili yake na kumfurahisha moyo wake pia. “Ukweli napenda mapenzi kuliko kitu chochote ila sipendi kuzinguliwa na wanaume, ninapenda muziki, filamu lakini haviwezi kufikia mapenzi kwani ndiyo kila kitu kwangu na yananipa starehe kuliko kitu chochote hapa duniani,” alisema Baby Madaha
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: