Huyu ndiye alie igiza muvi ya YESU, Mjue aliko kwa sasa na anafanya nini

Inaendelea,,,,,,, Baada ya filamu hiyo Briana anasema alirudi kuigiza majukwaani na kwenye runinga, ambapo kwa miaka zaidi ya 30 sasa tangu kutoka filamu ya Yesu tayari imetazamwa na watu zaidi ya bilioni tatu katika nchi 133 (kwa takwimu za mwaka 2001), zaidi ya watu milioni 117 waliamua kubadilisha maisha yao na kumpokea Yesu,filamu hiyo ambayo ilitengenezwa chini ya Campus Crusade for crusade ambao kwasasa wanaitwa Life Ministry pia nchini Tanzania wapo chini ya mkurugenzi Dismas Shekhalage.ambapo tayari imetafsiriwa katika lugha zaidi 500 huku nyingine zaidi ya 200 zikiwa njiani kutafsiriwa. Brian anawaambia watu kwamba yeye ni mwigizaji tu na sio Yesu kama watu wengine na kuwataka watu hao kujua hivyo ambapo anasema ameendelea kupata barua mbalimbali za kumpongeza na kumshukuru kwa kazi nzuri aliyofanya kwenye filamu hiyo,ambapo kwa upande wake anasema anayo nakala ya filamu hiyo kwenye maktaba yake nyumbani kwao Uingereza,ambapo kwa takribani miaka 20 filamu hiyo imekuwa ikitazamwa duniani kote na kubadilisha maisha ya watu. Kati ya filamu alizowahi kushiriki ni pamoja na A zed & Two Noughts ya mwaka 1985, The Feathered Serpent ya mwaka 1976-1978 na Tamthilia iitwayo Lillie iliyoigizwa mwaka 1978 akitumia jina la Frank Miles. Huyo ndiye Brian Deacon mwigizaji mkuu wa filamu ya ''JESUS''iliyoigizwa mwaka 1979 huko nchini Israel. Habari kwa msaada wa mtandao.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: