HANS POPPE: TUMEMALIZANA NA KESSI, CALABAR NAYE ANAKUJA
SIMBA SC imesema kwamba imefikia makubaliano na klabu ya Mtibwa Sugar juu ya mauziano ya beki wa kulia, Hassan Ramadhani Kessy.
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya Simba SC, Zacharia Hans Poppe ameiambia BIN ZUBEIRY jana kwamba, kikwazo cha kukamilisha dili la kumpata beki huyo kinda kimekwisha.
“Kikwazo kilikuwa ni klabu yake, Mtibwa Sugar, lakini sasa makubaliano yamefikiwa vizuri na kinachofuata ni kumsainisha mchezaji,”amesema Hans Poppe.
Hassan Kessy akimpitia Haruna Niyonzima wa Yanga SC
Mbali na hilo, Poppe amezungumzia beki wa kati, Mkenya David Owino ‘Calabar’ anayekuja kwa majaribio kutoka klabu ya ... sasa atawasili baadaye leo.
“Huyu mchezaji tunamjua, ni mzuri na anakuja ili tumuone tu mara moja kisha tujue kama tunamsajili au vipi,”amesema Poppe.
Amesema Nahodha wao pia, Mganda Joseph Owino naye anatarajiwa kuja leo, baada ya awali kukosa ndege. “Kuna tatizo sasa hivi la ndege kwa safari zetu za Afrika Mashariki, lakini nadhani limetatuliwa na Owino (Joseph) atatua kesho (leo),”amesema Poppe.@ bin zubery
0 comments:
Post a Comment