HABARI KAMILI KUHUSU KATIBU WA CHADEMA ALIYECHOMWA MSHALE HUKO MARA

KATIBU Mwenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Kata ya Rigicha Wilaya ya Serengeti mkoani Mara, Bahati Mayala, amelazwa hospitali Teule ya Nyerere DDH, kwa madai ya kuchomwa na kitu kinachodaiwa ni mshale eneo la mgongoni wakati anatoka kwenye mkutano wa kampeni Kijiji cha Kitembele. Mganga Mkuu wa hospitali ya Nyerere DDH, Dk. Kelvin Mwasha, alisema, walimpokea majeruhi huyo na kuanza kumpatia matibabu na hali yake ilikuwa inaendelea vema. Dk. Mwasha, alisema kuwa majeruhi huyo alipokelewa saa 6:00 Desemba 5 mwaka huu akiwa katika hali mbaya, ambako alifanyiwa upasuaji usiku huo na kuondoa mshale uliokuwa umeingia ndani sentimeta 6 na kukaribia kuathiri mapafu. Akisimulia mkasa huo kwa shida akiwa wodi ya wanaume alikolazwa kwa matibabu, Mayala alisema siku ya tukio alitoka kijijini kwake Rigicha na kwenda Kijiji jirani cha Kitembele kwa ajili ya kampeni za uchaguzi wa serikali za mitaa, ngazi ya vijiji, vitongoji. Alisema kabla ya mkutano wa kampeni kuanza, kulitokea vurugu na wafuasi wa vyama vingine, hata hivyo hali ilitulia na mkutano kuendelea na baada ya kumalizika aliondoka kurudi nyumbani akisindikizwa na wenyeji wake wa kijiji hicho, ambao waliamua kurudi baada ya mwendo kidogo. Alisema baada ya kuachana na viongozi wenzake, alipotembea umbali wa mita mia mbili hivi, majira ya saa 1:30 usiku katika kitongoji cha Ngayani, alisikia anapigwa na kitu mgongoni, alipogeuka aliwaona watu wawili aliowatambua wanakimbia, ambao ni Jumanne Milembe na Makanga Nyamandegele. Mayala, alifafanua kuwa baada ya tukio hilo alipiga yowe kuomba msaada ndipo watu jirani na eneo hilo walijitokeza kumsaidia na kubaini kitu kilichomchoma ni mshale na kumpeleka Kituo cha Polisi Issenye na kupewa PF 3. Mkuu wa Polisi Wilaya ya Serengeti, Pius Mboko, alisema Mayala alipigwa mshale wakati wanafuatilia wezi wa mifugo iliyoibwa katika kijiji cha Monuna
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: