CUF YAWAKABA KOO WAZIRI MKUU, TAMISEMI
Chama cha wananchi Cuf kimeibuka na kumtaka Rais Jakaya Kikwete kuwachukulia hatua Waziri mkuu Mizengo Pinda pamoja na Waziri wa Tamisemi Bi Hawa Ghasia kutokana na kushindwa kusimamia uchaguzi serikali za mitaa uliofanyika nchini siku ya jumapili desemba 14,2014.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa chama cha CUF taifa Prof Lipumba amesema kuwa kutokana na Tamisemi kushindwa kusimamia uchaguzi vizuri ni vema basi serikali ikabadilisha majukumu na kuipa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kusimamia mchakato mzima wa uchaguzi serikali za mitaa nchini Tanzania ili kuepuka kasoro zilizojitokeza katika uchaguzi huu.
Katika hatua nyingine mwenyekiti huyo amelitaka jeshi la Polisi kuacha kutumia nguvu katika vurugu zinapojitokeza wakati wa upigaji kura badala yake wafanye kazi kwa mujibu wa taaluma zao.
0 comments:
Post a Comment