CISSE AIANGAMIZA CHELSEA, MOURINHO NYWIII!!

MABAO mawili ya Papiss Cisse yameipa ushindi wa 2-1 Newcastle dhidi ya vinara wa Ligi Kuu ya England, Chelsea katika mchezo uliofanyika Uwanja wa St James' Park jioni hii. Katika mchezo huo ambao Steven Taylor alitolewa nje zikiwa zimebaki dakika 10 baada ya kuonyeshwa kadi ya pili ya njano, kipigo hicho kinakuwa cha kwanza kwa timu ya Jose Mourinho katika Ligi Kuu msimu huu. Cisse alifunga bao la kwanza dakika ya 57 na la pili dakika ya 78 kabla ya mkongwe Didier Drogba kuifungia Chelsea bao la kufutia machozi dakika ya 83.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: