CHADEMA YAWATAKA WENYEVITI WAPYA KUACHA UFISADI
Chama  cha  Demokrasia  na  Maendeleo  (CHADEMA)   kimewataka  wenyeviti  wote waliochaguliwa katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni  kuacha tabia ya kutumia ofisi za serikali kujinufaisha wenyewe.
Akizungumza katika mkutano uliofanyika jana Kimara Temboni Kata ya Msigani Naibu katibu mkuu Bara John Mnyika amewataka viongozi wote waliochaguliwa kupitia ukawa kutambua kuwa nafasi hizo zitumike katika kuwatumikia wananchi sio fulsa ya kufanya ufisadi na kuwanyanyasa watanzania.
Katika hatua nyingine  Mnyika amewashukuru wananchi wa eneo hilo kwa kuwapa fulsa ya kuwatumikia kwa miaka ijayo.
0 comments:
Post a Comment