Utalingoro Wanufaika na Pembejeo za Kilimo Kupitia Ushirika.

Utalingoro Wanufaika na Pembejeo za Kilimo Kupitia Ushirika. Utalingoro Wanufaika na Pembejeo za Kilimo Kupitia Ushirika. Wakulima wa kata ya Utalingoro wilaya ya Njombe, wameanza kunufaika na mfumo mpya wa serikali wa kutoa pembejeo za kilimo kupitia vyama vya ushirika, baada ya kuanza kukopa pembejeo za kilimo kwa bei nafuu kupitia chama chao cha kuweka na kukopa cha Twitangage Saccos. Wakulima walisema hayo katika mkutano wa kuchagua uongozi mpya wa Saccos hiyo na kueleza kuwa mfumo huo unawasaidia kuondoka na mfumo uliokuwepo wa kutumia mawakala ambao ulikuwa unawayumbisha wakuma. “Mfumo uliokuwa unatumiwa zamani na serikali wa mawakala ulikuiwa unatuyumbisha sana wakulima kutokana na baadhi yao kuchakachua mbolea lakini mfumo huu wa sasa unamjali mkulima na unamwezesha kupata mbolea anayohitaji badala ya mfumo ulikuwepo ambapo mkulima alikuwa analazimishwa kuchukua hata mbolea asiyohitaji,” alisema Senjawike. Rose Kitalima alisema: “Saccos yetu inatusaidia sana kuondokana na adha ya upatikanaji wa pembejeo za kilimo, kwa sababu ilifikia mahali paka wafanyabiashara wakawa wanachakachua mbolea wanatuuzia mchanga wa kutengenezea simenti wakitudanganya ni mbolea ya DAP, lakini kupitia mfumo huu hatutegemei kupata hasara kama hiyo.” Mwenyekiti wa bodi ya Saccos hiyo, Markus Ngole alisema mwanachama anaweza kupata pembejeo za kilimo kwa kununua moja kwa mojaau kwa kukopeshwa kwa riba nafuu na kwamba hata wakulima wengine walioko katika kata hiyo wateweza kununua pembejeo hizo kupitia bajrti hiyo. Kwa upande wake Mwenyekiti wa bodi ya mikopo wa Saccos hiyo Erasto Mpete alisema mfumo huo ni suluhisho pekee la kuondokana na malalamiko waliyokuwa nayo wakulimaya kupata pembejeo za ruzuku, hasa ya kupinga kupewa mbolea kwa kulazimishwa kuchukua mbolea ya minjingu amabayo walikuwa hawaitaki kutokana na kutotoa matokeo mazuri ya mazao. Alisema katika Saccos yao wanachama 400 watanufaika na mfumo huo huku wakitarajia idadi hiyo kuongezeka kutoka kwa wakulima wengine wasiokuwa wanachama wa Saccos hiyo kutaka kupata pembejeo hizo kupitia Saccos yao. Alisema kupitia mfumo huo mwanachama ataweza kununua au kukupa mbolea kwa asilimi mbili huku ada ya kiingilio ikiondolewa ili kuwawezesha wakulima kulima mazao ya kutosha na kupiga hatua kiuchumi, ambapo atarejesha mkopo huo kwa amu mbili kwa mwaka mwezi Novemba wakati wa mauzo ya mahindi na mwezi machi wakati wa mauzo ya viazi mviringo. Katika uchaguzi wa Saccos hiyo Ngole aliendelea kushilikilia kiti cha wenyekiti kwa kupata kura 65, makamu Mwenyekiti ni Richard na nafasi ya Mwenyekiti wa mikopo ikiendelea kuchukuliwa Erasto Mpete kwa kura 47.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: