UNAAMBIWA KUMLINDA MPENZI NI SAWA NA KULINDA SAMAKI BAHARINI… UKILINDA KIGAMBONI WENZAKO WANAVUA BAGAMOYO
Jamani wanawake wengine hawajielewi,
hawaelewi jinsi mahusiano yalivyo
complex.Ngoja niende direct tuende kwenye
point. Mke wangu ana tabia ambayo hakuna
mwanaume wa aina yoyote atamvumilia.
Nimechoka sasa ni muda muafaka wa action
najua iko siku atajuta kunifahamu.
Wote tunafanya kazi za kuajiriwa, hivyo
tunatoka asubuhi tunarudi jioni, japo yeye
anatangulia kurudi nyumbani. Sasa ana tabia
ya kubeba kila umbea anaopata kutoka kwa
mashosti zake na kuja kunisimulia mimi. Story
za nani anatembea na nani, mke wa nani ana
mahusiano na nani, mume wa nani anatembea
na nani, nani ana tabia gani etc. Mimi huwa
sina tabia ya kufuatilia maisha ya watu,
nimejiwekea commitment kwa kazi yangu na
familia yangu. Ya mtaani siyapi uzito, japo ni
muhimu kujua ABC za kitaa.
Moja, Kuna jirani yetu ana duka, mke wangu
akapata story kuwa yule mama na mumewe ni
waathirika. Mwenzangu akatangaza marufuku
kwenda kununua kitu chochote pale.
Nikamweleza kuwa kama ukimwi ungekuwa
unaambukizwa kwa style hiyo basi sijui kama
kuna binadamu angebaki hapa duniani.
Akaninunia.
Lingine linalofanana na hilo: Kuna siku alikuja
akanisimulia habari za mama mwingine
mwenye duka pale gengeni a.k.a. Mama J
ambaye hana mume alivyo na tabia mbaya,
Kuwa anawaingiza wanaume kwake
anawabadilisha tu. Sikutaka kupoteza muda
kwenye huo mjadala, kumbe yeye alitaka atoe
ultimatum kuwa ni marufuku kwenda kununua
bidhaa kwenye hilo duka. Siku moja
akaniomba nimsindikize tukachukue maziwa
mida ya jioni kwani mwenye kuuza hakuweza
kuleta. Wakati huo, tulikuwa tunatafuta mayai
ya kienyeji na upatikanaji wake ni wa shida.
Sasa tukiwa tunapita barabarani nikaona kwa
duka la mama J ana mayai ya kienyeji tena
mengi tuu. Saa ya kurudi nikashauri tuchukue
mayai, akasema twende nyumbani.
Nikamshawishi kwani upatikanaji wa mayai ni
shida, tukapitia pale tukachukua mayai kumi.
Pia nikanunua vocha ya tigo. Mama J
akasema vocha iliyobaki ni ya kurusha.
Nikamwambia poa nirushie, nikamtajia namba.
Kumbe hapo ndo nikawa nimetibua nyongo
bila kujua.
Tulipotoka pale njia nzima nikaona mtu
kanuna hataki kuongea. Kufika home kaniita
chumbani akaanza kunigombeza, eti mbona
alishaniambia tabia za yule mama alafu bado
naenda kununua vitu kwake?
Pili, nikipigiwa simu haijalishi ni muda gani na
ni wapi, lazima aulize nani amekupigia na
anasemaje. Ukweli hata nikimwambia hawezi
kumfahamu kila mtu na siyo kila kitu naweza
kumsimulia, mambo mengine ni ya kikazi. Kila
wakati anapekua simu yangu kana kwamba
niko polisi.
Tatu, tumebahatika kuwa na usafiri, na
tunapokaa daladala ni za shida kidogo. Hivyo,
kila asubuhi lazima tutoke wote, tumpitishe
mtoto shule, then nimdrop yeye kazini. Sasa
tukiwa njiani akimwona mtu yeyote
anayemfahamu ananiamrisha tumpe lifti huyo
mtu. Kumbuka mimi simwulizi kuwa huyo mtu
ni nani wake. Nachukulia kawaida. Sasa
ikitokea mimi nimemkuta mtu ninayemfahamu
au rafiki yangu, huyo mtu akishuka kwenye
gari, basi nitaulizwa maswali kama vile niko
polisi nahojiwa. Na bahati mbaya ikiwa ni
mwanamke, basi ananuna na wakati mwingine
nikitaka kusimama anasema twende bana
tunachelewa. Hii imenikera sana kuliko
kawaida.
Sasa, kuna shosti zake wa karibu sana, mara
nyingi nawapa lifti anapotoka kazini, basi
anawasifia sana kuwa wana tabia nzuri,
sometimes ananiomba tuwapeleke mpaka
mjini japo sina ratiba ya kwenda huko. Sasa
hao mashosti zake nimetembea nao na hajui. I
just wanted to prove kuwa mambo yake ya
kijinga hayanizuii kufanya nikiamua. Jamani
kumlinda mpenzi ni sawa na kulinda samaki
baharini, ukilinda Kigamboni wenzako
wanavua bagamoyo.
Anyway, nipeni wazo mbadala nimfanyeje ili
aelewe hilo somo?
0 comments:
Post a Comment