UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA, JESHI LA POLISI LATOA YA MOYONI
Jeshi la Polisi nchini Tanzania kupitia Wizara ya Mambo ya ndani ya nchi limesema kuwa linajipanga kuhakikisha kwamba uchaguzi wa serikali za mitaa unafanyika kwa amani na utulivu.
Kauli hiyo imetolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya ndani Bw. Mbarak Abdulwakil jijini arusha wakati wa mkutano wa baraza la wafanyakazi wa wizara hiyo.
Kwa mujbu wa Mkurugenzi wa Serikali za mitaa katika ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za mikoa na serikali za mitaa Bwana Kahrist Michael Luanda hivi karibuni amesema kwamba wananchi wanatakiwa kujiandikisha katika daftari la kudumu la wapiga kura kuanzia tarehe 23,11,2014 hadi tarehe 29,11,2014.
Uchaguzi wa serikali za mitaa utafanyika tarehe 14,12,2014 ambapo utahusisha uchaguzi wa wenyeviti wa vijiji, vitongoji, mitaa, wajumbe wa Halmshauri za vijiji na wajumbe wa kamati za mitaa.
0 comments:
Post a Comment