TATIZO KUBWA LINALOWASUMBUA WANAUME WAKATI WA KUFIKA KILELENI KATIKA TENDO LA NDOA, FAHAMU CHANZO NA TIBA
Ni ile hali ya mwanaume kushindwa kutoa manii nje wakati wa kufika kileleni badala yake manii kuingia katika kibofu cha mkojo,kwakawaida mwanaume anapofika kileleni shingo ya kibofu cha mkojo hujikaza na kufunga njia ya mkojo lakini kwa tatizo hili shingo ya kibofu cha mkojo huwa inashindwa kufunga hatimae kuruhusu uingiaji wa manii kwenye kibofu cha mkojo badala ya kutoka nje kupitia uume
Kuna matatizo mbalimbali ambayo yanapelekea mwanaume kuwa na tatizo hili;
i. Matibabu yanayohusu upusuaji wa shingo ya kibofu cha mkojo au tezi dume(prostate)yanaweza kupelekea misuli yashingo ya kibofu cha mkojo kutokuwa na uwezo wa kukaza vizuri ambapo ndo mwanzo wa tatizo
ii. Matokeo hasi ya baadhi ya madawa yanayotumika kutibu tatizo la presha ya kupanda yanaweza kusababisha misuli ya kibofu cha mkojo kupoteza uwezo wa kukaza vizuri
iii. Kuvimba kwa tezi dume(prostate enlargement)ni chanzo pia cha tatizo
iv. Ajali inayopelekea kuathirika kwa uti wa mgongo
v. Maambukizi ya bacteria au virus mbalimbali wanao shambulia kibofu cha mkojo au tezi dume wanaweza wakapelekea mwanaume akawa na tatizo hili
vi. Kuharibika kwa mishipa ya fahamu(nerve damage)kwa sababu mbalimbali eg.tatizo la sukari ya kupanda(diabetes mellitus)linaweza likapelekea nerve zinazo ratibu kufunga na kufunguka kwa shingo ya kibofu cha mkojo zisifanye kazi zake vizuri nakusababisha shingo ya kibofu cha mkojo kushindwa kufunga wakati mwanaume akiwa anafika kileleni nakupelekea retrograde ejaculation
DALILI ZA HILI TATIZO
Hili tatizo la RETROGRADE EJACULATION haliwezi kuathiri usimamaji wa uume na kufika kileleni lakini mwanaume kila anapofika kileleni manii yanaingia kwenye kibofu cha mkojo badala ya kutoka nje,dalili zingine zinazo ambatana na hii dalili kuu ni;
Kutoa manii kidogo au kushindwa kabisa kutoa manii wakati wakufika kileleni
Kutoa manii ambayo yamechanganyika na manii
Kuchukua mda mrefu kwa mwanaume au kushindwa kusababisha ujauzito kwa mwenzi wake zaidi ya mwaka mmoja pasipo kutumia kinga ya aina yeyote eg.condom
MATIBABU YA HILI TATIZO
Matibabu yapo lakini yanategemea chanzo cha tatizo na ukubwa wa tatizo,kwa mwanaume yeyote mwenye dalili kama hizo wahi hospitali kwa ajili ya uchiunguzi fika VICTORIA THERAPIES iliyopo mtoni kijichi kwa ajili ya vipimo,matibabu na ushauri jinsi ya kuondokana na hili tatizo au piga 0658027027 kwa ajili ya ushauri na maelekezo zaidi
MATOKEO ENDAPO MWANAUME ATACHELEWA KUPATA MATIBABU
Ugumba kwa mwanaume
Kushindwa kupata raha wakati wa kufika kileleni
Mwanaume kushindwa kujiamini kwa kuogopa kushindwa kutoa manii wakati wa kushiriki tendo la ndoa.
0 comments:
Post a Comment