MVURUGANO ACT, WALIOTIMULIWA WAWA MBOGO
Katibu Mkuu wa chama cha ACT-Tanzanua Samson Mwigamba anayedaiwa kufukuzwa.
Mvurugano umetokea katika chama kipya cha ACT-Tanzania ambapo siku ya jana waasisi wa chama hicho wametangaza kumfukuza katibu mkuu wa chama hicho Bw. Samson Mwigamba.
Chama hicho leo kimekanusha uamuzi huo wa kufukuzwa Bw. Mwigamba na kusema kwamba waasisi hao wamefanya mkutano ambao haukuwa na Baraka za chama hicho.
Waasisi waliotangaza kumfukuza Bw. Mwigamba ni Leopold Mahona ambaye ni naibu katibu mkuu bara na Greyson nyakarungu ambaye ni mwenyekiti wa ngome ya vijana. Waasisi hao wamefikia hatua hiyo kufuatia kinachotajwa ni mgogoro wa kisiasa ndani ya chama kati ya wanaojiita waasisi wa chama na viongozi wakuu wa chama na kupelekea kutoa tamko la kumsimamisha katibu mkuu na muhasibu wa chama.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo na idara ya mawasiliano na uenezi taifa wa chama cha ACT-Tanzania umesema kwamba, baada ya chama kupata usajili kimefanya vikao vya kamati kuu vitatu na pia kikao cha halmashauri kuu kimoja vikao vyote hivyo vimejadili mikakati na maendeleo ya chama hakuna kikao kilichojadili mgogoro ndani ya chama kwa sababu hakuna mgogoro.
Katika hatua nyingine taarifa hiyo imesema kwamba katibu mkuu na muhasibu hawajasimamishwa na kikao chochote cha chama. Pia taarifa hiyo imedai kwamba mkutano huo haukuwa na baraka za chama hicho badala yake kimeyapokea malalamiko yao na watayatolea tamko
0 comments:
Post a Comment