SAKATA LA ESCROW: VIGOGO WA PAC MATATANI
Ikiwa ni muda wa lala salama umebaki kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanza kujadili ripoti ya uchunguzi wa IPTL kuhusu ufisadi katika akaunti ya Escrow. Mwenyekiti wa kamati PAC Zitto Kabwe ameibuka na madai kwamba maisha yao yako matatani kufuatia kutishwa na wanao tuhumiwa katika sakata hilo.
Kwa mujibu wa Mwenyekti huyo kutoka Bungeni mjini Dodoma amebainisha kwamba Usalama wa wajumbe wote wa PAC upo shakani hivi sasa ambapo bunge linatarajia kuanza uwasilishwaji ripoti hiyo kesho.
Kutokana na vitisho hivyo Bw. Zitto Kabwe amesema, kamwe hawezi kuogopa vitisho kwa kuwa maisha yake ameyaweka nadhiri siku nyingi kutokana na kusimamia ukweli unao onekana kuwa kikwazo kwa watendaji serikalini ambao ni Mafisadi. Zipo taarifa nyingine kwamba kuna vipeperushi vimesambazwa kwa lengo kumchafua suala ambalo amesema halina tija kwake.
Sakata la IPTL linatokana na Ripoti ya Tegeta Escrow inayotokana na uchunguzi maalumu wa Sh 306 Bilioni zilizochotwa katika akaunti ya Escrow ndani ya Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Kesho (jumatano) ni siku ambayo watanzania na Dunia kwa ujumla wanaisubiri kwa hamu ili waweze kujua nini hatma ya fedha za umma zilizotafunwa na vigogo wasio waadilifu, pamoja na wale wanao kesha kuhakikisha kwamba wanakwamisha uwasilishaji huo kwa njia mbalimbali ikiwemo kuvujisha ripoti ya IPTL.
0 comments:
Post a Comment