WARIOBA AWAMALIZA CCM ‘MASLAHI’ KATIKA KATIBA MPYA

Mdahalo wa katiba umefanyika majira leo katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam ambapo aliyekuwa mwenyekiti wa mabadiliko ya tume katiba, Jaji Warioba ameibuka na kubainisha kwamba katika mchakato wa katiba kuna makundi mawili yameibuka ndani ya CCM ambayo ni Chama cha Mapinduzi (CCM) imara pamoja na CCM maslahi. Akizungumza katika mdahalo hu wa katiba kuhusiana na tofauti iliyopo kati ya katiba iliyopendekezwa bungeni na katiba iliyopendekezwa na tume yake amesema, suala la maadili ni moja ya suala nyeti lililoachwa na wabunge wa Bunge maalumu la katiba ndio maana hivi sasa kuna sakata Escrow ikiwa ni matokeo ya viongozi kutokuwa na maadili. Kuhusu viongozi kuwa na akaunti nje ya nchi wananchi walitaka viongozi wote wa umma wasiwe na akaunti nje ya nchi kutokana na kukithiri viongozi wanaotorosha fedha na kuzificha nje ya nchi na hivyo kukosesha mapato ya nchi. Kipengele ambacho nacho kimetupwa na wabunge hao. Naye Humphrey Pole akizungumzia kuachwa kipengele muhimu cha kuwawajibisha wabunge kilichoachwa na wajumbe wa Bunge maalumu la katiba amesema kwamba nchi zote duniani zina utaratibu wa kuwajijibisha Wabunge ili kuongeza tija katika utendaji kazi wao. kuondoa kipengele hicho ni sawa na kuwafanya wabunge kufanya kazi kwa mfumo wa bora liende. Ameongeza kwamba elimu ya mbunge waliyoweka katika iliyopendekezwa ni kujua kusoma na kuandika wakati Waziri anatakiwa awe na Shahada, je ikiwa wananchi watawachagua wabunge wasio na shahada baraza la Mawaziri litaundwaje?. Kwa upande mwingine, Jaji Warioba ameshangaa mawaziri na viongozi wengine kuipigia chapuo katiba iliyopendekezwa wakati huo katiba ni wananchi je kuna nini hapo?, Ameoimba serikali kuhakikisha kwamba inawagawia wananchi katiba iliyopendekezwa ili waisome na kuielewa na sio kushawishiwa na wanasiasa pamoja na watendaji wenye maslahi yao.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: