MSF kujaribu tiba mpya dhidi ya Ebola

Shirika la Madaktari wasio na mipaka, MSF limesema litafanya majaribio ya tiba mpya ya Ebola katika vituo vitatu Afrika Magharibi. Wafanyakazi hao watatumia dawa aina mbili zilizoainishwa na Shirika la Afya duniani, WHO. Sababu ya kufanyika kwa majaribio hayo ni kuwafanya Wagonjwa kuendelea kuwa hai wakati wa siku 14 za mwanzo tangu maambukizi ya ugonjwa huo. Taarifa hii inakuja wakati idadi ya waliopoteza maisha kutokana na Ebola kufikia 5,160. Ugonjwa huo umeelezwa kuathiri zaidi ya watu 14,000, karibu wote kutoka Afrika Magharibi. Msemaji wa MSF Annick Antierens amesema hatua hiyo mpya inafanywa kwa kushirikiana na watafiti kutoka Uingereza,Ufaransa na Ubelgiji kwa lengo la kutoa nafasi ya waathirika kuwa na matumaini ya kuishi
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: