MIKOA INAYOONGOZA KWA UKIMWI TANZANIA HII HAPA

Mwenyekiti mtendaji kutoka tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt Fatma H. Mrisho akihutubia wakati wa mkutano wa serikali na wadau wa ukimwi. Wadau mbalimbali waliohudhuria mkutano wa serikali unaohusu wadau wa ukimwi. Serikali kupitia tume ya Taifa ya kudhibiti ukimwi imeweka mikakati pamoja na kusimamia juhudi zinazofanywa na kuendelezwa na wadau kuhusu masuala ya ukimwi kuhakikisha kuwa maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi yanafikia sifuri. Hayo yamesemwa na Mwenyekiti mtendaji kutoka tume ya kudhibiti ukimwi Tanzania (TACAIDS) Dkt Fatma H. Mrisho wakati wa mkutano wa serikali na wadau wa ukimwi kupitia utekelezaji programu za ukimwi jijini Dar es salaam. Ameongeza kuwa maambukizi ya ukimwi yamepungua ukilinganisha na miaka 10 iliyopita ambapo idadi imepungua kutoka waathirika laki moja na elfu themanini hadi kufikia waathirika elfu sabini na mbili kwa sasa. Katika hatua nyingine mikoa ya Njombe, Shinyanga, Dares salaam, Mbeya na Rukwa ni mikoa yenye idadi kubwa ya watu wenye virusi vya ukimwi nchini Tanzania. Kwa upande mwingine Dkt Fatma amewataka wadau wa ukimwi kutoka mikoa hiyo kuongeza elimu kwa jamii ili kupunguza maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi pamoja na magonjwa ya zinaa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: