dereva toyo

Inaendelea "duuuuu kweli huku ndio kutekwa kweli" "na hio pesa ni shing ngapi?" "hiii? aaa hii ni ndogo tu" "kiasi gani?.... haaa pesa yote hiii ndio kakulipa kwani ana sherehe?" "ah ah ni yeye tu" "sasa Aaayaaaa Yaani we unaniuzi wewe hebu twende uko" Nilipokua naondoka nilimuangalia nesi wa watu anatia huruma huyo duuuu Ila nilimfariji kwa kuandika sifuri heweni na kugusa kichwa changu.... kumaanisha kua ile namba nimeishika kichwani...... kwahio hata alivyochana ni kama kajisumbua tu... maana kichwa yangu haioni kitu mara mbili imenasa... Basi tulitoka hadi nje na kupanda gari Lakini saa hio nilikua nina hasira hio duuu..... Aliwasha gari na kuondoka mahari nisipo pajua kua tunaelekea wapi... Alifika mahari Akasimamisha gari kisha akaniambia nishuke "shuka" "ndio tumefika au?" "shukaaaaaaaa" "sasa si nimekuuliza tu" "hutaki kushuka au?" "mmhh basi mama nashuka ee?" Nilishuka na kusimama pembeni ili nimsubiri aje.... Mara alitimua mbio huku nikiona vumbi tu...sioni hata gari Sasa nikabaki na maswali kua hio kesi imeisha ishaje? Maana ni kama kaniacha njia ya panda.. ila kikubwa ni kwamba nipo huru tu hivyo niliita toyo na kunipeleka hadi nyumbani kisha kisha nikachukua mkoba wangu na kuelekea studio kusafisha picha za nesi HASNA daahh nesi kumbe ni mtoto wa liislamu bwana ila ni mlaini na mzuri wa hipsi hadi raha yani....... BAADA YA WIKI MBILI KUPITA Na leo ni siku nyingine tena nikiwa nyumbani... na kazi yangu ya udereva toyo ushaanza tayari..Sasa leo nilikua nyumbani na wazee wangu wakinishauri kitu "mwanangu sasa si uoe?" "duuu mama na maisha haya nioe kweli?" "maisha gani na una kazi jamani?" "aaaa mama subiri kwanza.... maana kazi yenyewe ina wiki mbili tu mamaa" "haya je huu mwezi ukiisha?" "labda miezi miwili ipite kwanza" "nini? mwezi huu tu utaoa nakwambia labda niwe sio mama ako niliokuza" "eeeeh yamekua hayo tena mamaa?" SAMAHANINI SANA WATU WANGU KWA HIZO HERUFU ZINAZOONGEZEKA KAMA HIO "MAMAA" KWANI SISI WATOTO WA ARUSHA HUA NDIO RAFUDHI YETU YA KUONGEZA HERUFI NYINGINE MBELE YAKE.... HIVYO UKIONA NENO "MAMAA" BASI UJUE NI "MAMA" AU UKIONA NENO "BARAKAA" BASI UJUE NI BARAKA... HIVYO USIJE SEMA SIJUI KUANDIKA BURE..... MAANA NI UZOEFU WA RAFUDHI YA KICHUGA CHUGA........ "ndio....tena kesho kutwa pangisha chumba chako.....tena pale kwa mama nusura kuna chumba cha umeme ni kizuri kodi ni shilingi elfu 20 tu" "duuuuu kweli mmenichoka aisee" "unasemaje? we pumbavu njoo mwenyewe....yaani nisikuchoke ukiwa tumboni.... na kuninyea na usumbufu wa utotoni kwako nikuchoke sasa hivi?" "nisamee mamaa" "njooo nakwambia pumbavu wewe" Mara baba kaja huku kanuna buyo "ana nini mbona mnagombana?" "yaani huyu mtoto ananiambia eti tumemchoka?" "kwanini aseme hivyo?" "Eti kisa nimemwambia apangishe chumba chake" "Huyu mtoto ni mpumbavu kweli... hebu mlete hapa nimnyooshe mshenzi huyu.... yaani alivyonisumbua utotoni huyu leo useme tumekuchoka..... tena hakuna mtoto alionisumbua kama wewe pumbavu mkubwa wewe" "ayaaaaa mzeee basi mzeee utaniumiza huku mzee" "wewe baba jimi usimpige huko bwana wewe" "wacha nimpige huko huko maana toka aanze hio toyo yake amekua mtu wa wanawake kila siku huyu....maana juzi nilimkuta kasimama na mwanamke mkubwa kuliko hata wewe mama ake?" "haaaaaaa unasemaje baba jimi?" "ndio hivyo" "mungu wangu we mtoto sijui nikupige wapi we mwana haramu mkubwa wewe" Sasa mama alipandisha mori kuskia nilikutwa na jimama kuliko yeye... Mara mama kanyanyua panga lile la mzeee... linawaka waka kwa ukali wake..... "heeee we mama jemsi panga la nini tena?
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: