BUNGENI: SERIKALI YAIKANA VIKOBA, YASEMA HAINA BAJETI YAKE

Leo Bunge linaendelea na vikao vyake ambapo asubuhi hii ni kipindi cha maswali na majibu. Katika kipindi cha maswali na majibu Mbunge wa Rungwe Profesa David HomeliMwakyusa ameuliza,tangu kuanzishwa kwa VIKOBA wananchi wamenufaika sana, Je Serikali inaitambua VICOBA kama ni mkombozi kwa wananchi vijijini? Akijibu swali hilo Naibu Waziri wa Fedha Ndugu Mwigulu Nchemba amekiri kwamba VIKOBA ni miongoni mwa taasisi ndogondogo za fedha zinazoanzishwa ili kutatua changamoto za kifedha kwa wananchi hususan wa vijijini. Ameongeza kuwa taasisi hizi husimamiwa na wananchi wenyewe na kuthibitisha kuwa VIKOBA si taasisi ya Serikali kama ambavyo baadhi ya watu wamekuwa wakidhani. Hata hvyo Ndugu Nchemba amebainisha kwamba serikali kupitia wizara ya fedha haina bajeti kwa taasisi ya VICOBA hapa nchini Tanzania.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: