ASKOFU KILAINI AFUNGUKA SAKATA LA WIZI FEDHA ZA ESCROW
Askofu Msaidizi wa Jimbo la Bukoba anayejulikana kama Methodius Kilaini amefunguka kuhusiana na sakata la wizi fedha Ecsrow ambapo anadaiwa kupata mgawo wa shilingi milioni 80.5 kutoka kwa mkurugenzi mkuu wa Kampuni ya VIP Engineerin Ndugu James Rugemalira.
Akizungumza kwa njia ya simu na Mwandishi wetu Askofu huyo amebainisha kwamba sio mara yake ya kwanza kupokea kutoka kwa mfanyabiashara huyo kutokana na mfanyabiashara huyo kuwa mara kadhaa amekuwa akichangia miradi ya kanisa hilo.
Hatua hiyo inatokana na Mwenyekti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za serikali (PAC) iliyomtaja kuwa ni kati ya viongozi walipota mgawo wa fedha za Escrow zilizotokana na kuwepo mgogoro baina ya Kampuni ya Kufua Umeme ya IPTL na Shirika la Umeme la Tanzania (Tanesco).
Viongozi wengine wa dini wanaotuhumiwa kupokea mgawo katika sakata hilo ni Askofu Eusebius Nzigirwa aliyepata kiasi cha shilingi milioni 40.4 pamoja na Padre Alphonce Twimanye Simoni kiasi cha shilingi milioni 40.4
0 comments:
Post a Comment