ARUSHA, MANYARA, TANGA VINARA WA NOTI BANDIA, BOT YAWEKA BAYANA
Uwepo wa fedha nyingi bandia hapa nchini umechangia kupunguza thamani ya fedha halisi na kupelekea kuwepo kwa mfumuko wa bei kwa kuongeza fedha iliyopo kwenye mzunguko.
Akizungumza katika kikao cha dharura cha Kamati ya Ushauri ya mkoa wa Kilimanjaro (RCC), Mkurugenzi wa benki kuu ya Tanzania Tawi la Arusha Said Chiguma, alisema nchi imekuwa ikikabiliwa na tatizo kubwa la uingizwaji wa fedha bandia jambo, ambalo limesababisha baadhi ya fedha hizo kuingizwa kwenye mzunguko huo.
Alisema kuwa miongoni mwa mikoa ambayo imeathirika na uwepo wa fedha hizo ni pamoja na Mkoa wa Arusha ambao unaongoza kwa kuwa na idadi kubwa ya noti bandia za shilingi 10,000 kwa kuwa na jumla ya noti bandia 102 na noti za shilingi 5,000 jumla ya noti bandia 23 sawa na asilima 54.8 kwa kipindi cha Julai 2013 hadi juni 2014.
Chiguma aliongeza kusema mkoa ambao unafuatia kwa kuwa na fedha badia ni mkoa wa Manyara ambao una noti za shilingi 10,000 noti 84 ambazo ni sawa na asilimia 36.9.
Hata hivyo Chiguma alitoa rai kwa wananchi waliopo katika Kanda ya Kaskazini kuwa makini pindi wanapopokea fedha hususani nyakati za usiku.
Aidha alisema takwimu hizo zinatokana na matukio yaliyoripotiwa katika vituo vya polisi ambapo kwa upande wa fedha bandia zilizopatikana kutoka katika benki za biashara kwa Mikoa wa Arusha unaongoza kwa kuwa na jumla ya noti bandia 426 ambayo sawa na asilimia 55.9
Alifafanua kuwa,Mkoa unaoshika nafasi ya tatu ni Mkoa wa Tanga,kutokana na kuwa na matukio ya noti bandia za shilingi 10,000 na 5,000 ambazo ni 173 sawa na asilimia 22.7 ikifuatiwa na Mkoa wa Kilimanjaro kwa kuwa na jumla ya noti bandia 162 sawa na asilimia 21.4 kwa kipindi cha mwaka 2013/2014.
credit;jaizmelaleo blog
0 comments:
Post a Comment