UHABA WA NYUMBA ZA WALIMU WASABABISHA MWALIMU KUISHI DARASAN

Uhaba wa nyumba za walimu katika Shule ya sekondari Ikovo iliyopo katika kata ya Ludende wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe umepelekea mwalimu mmoja kuishi darasani na wengine kulazimika kuishi umbali wa zaidi ya kilometa 5 na shule hiyo ya kata hali ambayo imekuwa ikiwavunja moyo walimu hao katika utendaji kazi. Akisoma risala katika mahafari ya kidato cha nne katika shule hiyo yaliyofanyika hivi karibuni Mwalimu mkuu wa shule hiyo Rezile Mtweve alisema shule hiyo inachangamoto nyingi lakini kubwa ni ile ya ukosefu wa nyumba za kutosha walimu hali ambayo imepelekea mwalimu mmoja kuishi katika moja ya mdarasa na wengine kuishi mbali na eneo la shule. Mwalimu Mtweve alisema alilazimika kumruhusu mwalimu huyo kuishi katika moja ya madarasa kutokana na hali halisi ya mazingira ya kijiji cha Ludende kuwa mbali na shule hiyo ambapo walimu wanaoishi kwa wananchi wanalazimika kutembea kwa miguu umbali mrefu unaozidi kilomita 5 hadi kufika shuleni hapo hivyo inakuwa vigumu kuwahi katika vipindi. “tunazo nyumba ambazo bado hazijapauliwa wala kukarabatiwa hali ambayo inawakatisha tamaa ya kufanya kazi baadhi ya walimu wanaopangiwa katika shule hii na pia hata wanafunzi wamekuwa watoro katika masomo kutokana na walimu kutumia muda mwingi wa kutembea na kusababisha kuchoka kabla ya kuanza vipindi”,alisema Mwalimu Mtweve. Alisema utoro huo umekithiri kwani wanafunzi wanaohitimu walianza kidato cha kwanza mwaka 2011 wakiwa wanafunzi 69(wavulana 38 na wasichana 31)lakini mpaka wanahitimu wamebaki wanafunzi 18(wavulana 09 na wasichana 09)ndio wanaotarajia kufanya mtihani hali ambayo imekuwa mbaya zaidi licha ya kuwa shule hiyo imekuwa na walimu 18 mpaka sasa. Changamoto nyingine zinazo ikabiri shule ya Sekondari Ikovo ni upungufu wa walimu wa masomo ya Sayansi,ukumbi wa mikutanao,baadhi ya wazazi kutoelewa umuhimu wa elimu,mimba kwa wanafunzi wa kike,wazazi na walezi kutolipa michango na ada kwa wakati,kutokuwa na nishati ya umeme kwaajili ya kusoma wanafunzi nyakati za usiku licha ya kuwa tasaf walitoa fedha kwaajili ya kununua sola lakini hakuna nishati hiyo mpaka leo. Akitoa hotuba katika mahafari hayo Mgeni rasmi ambaye ni mfanyabiasha wilayani Ludewa na mzawa wa kata hiyo Bw.Huruma Mgaya alikili kuwepo kwa changamoto hizo kutokana na hali halisi aliyoiona wakati akioneshwa majengo na mazingira ya shule hiyo kabla ya sherehe kuanza na kubaini mapungufu makubwa ya wazazi wa kata hiyo kwa kutoshirikiana na walimu ipasavyo katika kupuzipunguza changamoto hizo. Bw.Mgaya aliwataka wazazi kushirikiana na walimu ili kuhakikisha tabia ya utoro wa wanafunzi inakoma shuleni hapo kwani wazazi wamekuwa nyuma katika kufuatilia maendeleo ya watoto wao wawapo shuleni hali inayosababisha baadhi ya watoto kutohudhuria masomo na kuishia vichakani. Kuhusu suala la numba za walimu Bw.Mgaya alishangazo na kitendo cha kuona baadhi ya nyumba zimejengwa na hatua iliyobaki ni kupaua na kuzipiga bati hatimaye kuzikarabati lakini kila kitu kipo kinachoshindikana ni ukosefu wa mafundi na misumari ya kenji na bati hali ambayo si sahihi kwani kata hiyo inamafundi wengi hivyo viongozi wanatakiwa kufanya jambo ili mafundi hao wafanye kazi hizo. Bw.Mgaya alisema Mbunge wa jimbo la Ludewa Mh.Deo Filikunjombe alitoa mabati 200 na mifuko ya saruji 200 lakini cha kushangaza mpaka sasa vifaa hivyo havijafanyiwa kazi na kupelekea walimu kuishi madarasani hivyo aliwaahidi kutoa misumari ya kenji na bati ili nyumba hizo zimalizike haraka na kuwahamisha walimu wanaoishi madarasani na mbali na eneo la shule ili waishi katika nyumba zao. Aidha aliwataka wazazi kuwahimiza watoto wao kuzingatiz masomo na kuacha utoro kwani hakuna urithi kwa mtoto Duniani zaidi ya elimu pia kuwatunza walimu wanaofanya kazi katika shule hiyo kwani kunashule bado zinatatizo kubwa na uhaba wa walimu tofauti na shule hiyo yenye walimu 18 wakiwemo wanawake 2 na wanaume 16 wakiwa na upungufu wa mwalimu mmoja wa masomo ya Sayansi. Mwisho.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: