TANZANIA YAPAA VIWANGO VYA UBORA FIFA

Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars leo imepanda kwenye viwango vya ubora wa Shirikisho la Mpira wa miguu Duniani FIFA kwa nafasi tano zaidi kufatia ushindi wa bao 4-1 iliyoupata dhidi ya Benin wiki Mbili zilizopita katika Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam. Kwa matokeo hayo Tanzania sasa inakuwa imepaa hadi nafasi ya 110 kwa kufikisha pointi 291 tofauti na mwezi jana ambapo ilikuwa ya 115 katika viwango vya ubora Duniani. Kwa upande wa majirani zake Kenya na Uganda wao wameporomoka kwa nafasi 5 kila mmoja Kenya kutoka 111 hadi 116 wakati Uganda wao wamedondoka kutoka 79 hadi nafasi ya 84. Licha ya matokeo hayo lakini Uganda wameendelea kuwa juu kwa ukanda wa Afrika Mashariki na kati. Kwa upande wa kilele cha Afrika Algeria inaongoza baada ya kuanda kwa nafasi tano hadi namba 15 Duniani ikiwa ya kwanza Afrika nyuma yake ni Ivory Coast pamoja na Ghana. Nayo Timu ya Taifa ya Ujermani imeendelea kuongoza kwa ubora wa viwango Duniani kwa kushika nafasi ya kwanza ikifatiwana Argentina pamoja na Colombia huku Brazil ikiwa ya sita Ufaransa wakishika nafas ya Saba
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: