Simba yapania kuua bundi wa mkosi, Yanga vitani na Stand United

Kimuhemuhe cha ligi kuu ya soka Tanzania Bara kitaendelea siku ya Jumamosi huku vigogo Simba na Yanga wakipania ushindi kwa hali mali baada ya mapumziko ya juma moja. Simba, iliyotoka sare ya nne ya bila kufungana Jumamosi iliyopita dhidi ya watani wake wa jadi Yanga na kuendelea kusuasua katika mawindo ya kushinda taji hilo, itaikwaa timu ya Magereza (Prisons) katika uwanja wa Sokoine mjini Mbeya. Kocha Mzambia, Patrick Phiri, aliyeweka rekodi klabuni hapo ya kuchukua ubingwa bila kufungwa katika msimu wa mwaka 2009/2010, amesema ana imani wataoweza kushinda mechi hiyo ya ugenini ili kumuondoa bundi anayewanyima ushindi na kupata pointi tatu. Simba ina pointi nne tu, baada ya kupata sare nne dhidi ya mabingwa wa ligi mwaka 1988, Coastal Union, Polisi Morogoro,Stand United na mahasimu wake Yanga. Yanga, chini ya kocha wa zamani wa timu ya taifa, Taifa Stars, Marcio Maximo,itakuwa na kibarua kigumu huko ugenini, Shinyanga, dhidi ya Stand United, inayoshiriki ligi kuu kwa mara ya kwanza. Ikiongozwa na wachezaji wake mahiri kama vile Wabrazil Coutinho na Jaja na mfukuza upepo, Mrisho Ngasa, pia itaelekea Bukoba kuvaana na Kagera Sugar Novemba mosi
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: