Phiri anunua staa Jangwani

KOCHA wa Simba, Patrick Phiri, amepanga kufumua kikosi chake katika usajili wa dirisha dogo hapo Desemba ambapo ametamka kuwa anahitaji kuwa na makipa wanne wenye ushindani mkubwa na kusisitiza ni lazima afanye uamuzi mgumu juu ya hilo huku akitaka uongozi umnunulie kipa wa Yanga, Juma Kaseja. Kwa sasa Simba ina makipa watatu; Ivo Mapunda, Hussein Sharif ‘Casillas’ na Manyika Peter ambaye usajili wake ni wa U-20. Hiyo inamaanisha kwamba Kaseja akitua Simba uwezekano wa Mapunda kurejea Ligi Kuu Kenya ni mkubwa kama ilivyoanza kuvumishwa kwani Simba itakuwa na makipa wanne na nafasi yake kucheza itakuwa finyu. Phiri ameliambia Mwanaspoti kuwa alipatwa na wakati mgumu baada ya makipa wake wawili kuumia Ivo na Casillas na kubakiwa na mmoja tu Manyika ambaye hata hivyo alionyesha kiwango cha juu katika mechi yao na Yanga iliyochezwa Jumamosi iliyopita na kutoka suluhu. Baada ya mechi hiyo, Phiri alisema kuwa Manyika ana kiwango kikubwa lakini anahitaji awepo na kipa mbadala huku akitamani kumnasa Kaseja ambaye aliwahi kuidakia Simba kwa miaka 10. “Binafsi huwa namkubali Kaseja kuwa ni kipa bora kutokana na uwezo wake wa kudaka, ningependa kuwa naye kwani nimewahi kumfundisha na ninajua uwezo wake, nina makipa watatu ambao ni wazuri lakini kuelekea mechi ya Yanga wawili walikuwa na majeruhi, nilikuwa katika wakati mgumu ingawa nilimwamini Manyika,” Phiri alisema. “Nikisajili kipa mzoefu itanibidi niwe na uamuzi mgumu katika upangaji kwani ni lazima nikimtumia Manyika kutokana na uwezo aliokuwa nao, nikimkalisha benchi nitaua kiwango chake, atakuwepo kipa namba moja lakini wote watadaka kulingana na mechi zilivyo.” Kaseja kwa sasa hapati nafasi ya kudaka katika kikosi cha Yanga kwani kocha Marcio Maximo amemwamini kipa Deo Munishi ‘Dida’. Kuhusu safu ya ulinzi, Phiri alisema: “Pale kati Joseph Owino na Hassan Isihaka wanatosha sina haja ya kusajili, lakini beki wa pembeni ndio kuna tatizo kwani wapinzani wetu wamegundua tatizo hilo, hivyo nitaimarisha pembeni, kiungo mkabaji ambapo kwa sasa namtegemea sana Jonas Mkude. Nitaongeza na straika mmoja.” Kwa hesabu za Phiri basi uongozi wa Simba ambao msimu huu umesajili wachezaji 29 na kubakiwa na nafasi moja ili wafike 30 watalazimika kupunguza baadhi ya wachezaji wao ili wasajili wachezaji ambao kocha atapendekeza katika nafasi husika. Phiri aliongeza: “Matokeo haya (mfululizo wa sare) sio mazuri kabisa kwetu, tunahitaji ushindi, lakini pia ni bora tumetoka sare na Yanga kuliko wangetufunga maana ingeleta shida zaidi, tunaenda kucheza na Prisons ambao sijawaona uwezo wao hivyo lazima niongeze mbinu za kiufundi kuhakikisha ushindi ugenini unapatikana.” Simba ilianza mazoezi yake jana Jumatatu jioni, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam source,,mwana spot
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: