LIGI KUU TANZANIA BARA MOTO WAZID KUWAKA

LIGI Kuu ya Tanzania bara mzunguko wa nne iliendelea tena wikiendi hii kwa timu 14 kushuka katika viwanja tofauti kuwania pointi tatu. Pambano kubwa katika wiki hii lilipigwa uwanja wa taifa Dar es Salaam,ambapo mahasimu wa jadi Yanga na Simba walikutana Jumamosi na kutoka sare ya bila kufungana. Pambano hilo lililotia for a kwa kuhudhuriwa na mashabiki wengi kuliko mechi zote ambazo zimefanyika msimu huu ilishuhudiwa timu hizo zikigawana muda kwa kucheza Simba iliyokuwa ugenini ilicheza vizuri kipindi cha kwanza na Yanga ikafanya hivyo kipindi cha pila lakini hakuna timu iliyopata goli. Matokeo hayo yameifanya Yanga kufikisha pointi saba katika michezo minne iliyocheza msimu huu huku mahasimu wao Simba ikifikisha pointi nne katika mechi nne huku ikiwa haijawahi kushinda hata mechi moja msimu huu. Mchezo mwingine uliokuwa unafuatiliwa kwa karibu na mashabiki wa soka ni ule uliozikutanisha timu za Mbeya City dhidi ya Mabingwa watetezi Azam FC,uliochezwa Jumamosi kwenye uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya. Mabingwa watetezi Azam FC,walifanikiwa kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi baada ya kupata ushindi wa bao 1-0,ikiwa ugenini kwenye uwanja huo wa Sokoine huku bao hilo pekee likifungwa na nahodha wake wa zamani Agrrey Moris katika dakika ya 19. Ushindi huo umeifanya Azam kufikisha pointo 10 na idadi ya mechi 30 za kucheza bila kufungwa kwenye ligi kuu ya Tanzania bara tangu msimu uliopita ambapo waliweza kuchukua ubingwa bila kufungwa. Waliokuwa vinara kabla mechi za wikiendi hii Mtibwa Sugar Jumamosi walijikuta wakipunguzwa kasi yao na Polisi Moro baada ya kutoka sare ya bila kufungana mechi ikichezwa kwenye uwanja wa Jamuhuri mkoani Morogoro. Sare hiyo ya kwanza kwa vijana wa kocha Mecky Maxime,imewafanya kushika nafasi ya pili licha ya rekodi kuonyesha timu hiyo inalingana kilakitu na Azam ikiwepo magoli ya kufunga na kufungwa pamojoa na pointi. Wikendi ijayo Mtibwa Sugar itatoka kwa mara ya kwanza tangu kuanza kwa msimu huu ikielekea kwenye uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya kupambana na Mbeya City ambayo juzi Jumamosi imefungwa na Azam kwenye uwanja hu. Katika uwanja wa Nangwanda Sijaona kule Mtwara timu ngeni ya Ndanda FC,mambayo lizidi kuwawia magumu baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 na Ruvu Shooting mbele ya mashabiki waliokuwa wamejazana kwa wiki kuishuhudia timu yao kwa mara ya kwanza ikicheza nyumbani. Kipigo hicho ni cha tatu mfululizo kwa Ndanda FC,iliyoanza msimu huu kwa kishindo kufuatia kuifunga Stand United mabao 4-1 katika mchezo wa ufunguzi Septemba 20 kwenye uwanja wa Kambarage mkoani Shinyanga. Zipo habari za kuaminika kutoka Mtwara kuwa tayari uongozi wa Ndanda FC,umemtimua kocha wake Dennis Kitambi kufuatia matokeo hayo mabaya yanaoifanya timu hiyo kushika nafasi ya 13 ikiwa na pointi tatu kibindoni. Huo niushindi wa kwanza kwa Ruvu Shooting,inayonolewa na kocha Tom Alex Olaba,ambayo msimu huu ilianza vibaya kufuatia vipigo viwili mfululizo kutoka kwa Tanzania Prisons na Kagera Sugar, na baadaye kutoka sare na Mbeya City. Kwenye uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga,mabingwa wa mwaka 1988 Coastal Union,ilipata ushindi wa pili mfululizo msimu huu kwa kuifunga Mgambo JKT,mabao 2-1. Kocha wa Coastal Union Mkenya Yusuph Chipo,amewapongeza wachezaji wake kwa kujituma na kuhakikisha timu yake inaondoka na pointi zote tatu na kuifanya timu hiyo kuifikia Yanga katika nafasi ya tatu zikiwa na pointi saba. Katika uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba timu ya Kagera Sugar ikicheza nyumbani kwa mara ya kwanza ilishindwa kuutumia vyema uwanja huo baada ya kulazimishwa sare ya bila kufungana na Stand United ya Shinyanga. Sare hiyo imeifanya Kagera Sugar inayofundishwa na kocha Jackson Mayanja raia wa Uganda kufikisha pointi tano katika mechi nne ilizo cheza na kupoteza mmoja dhidi ya Mgambo JKT ya Tanga. Pia sare hiyo imeinufaisha Standa United ambayo sasa imefikisha pointi tano katika mechi nne ilizo cheza na mafanikio pekee ya kujivunia kwa timu hiyo ambayo wikiendi ijayo itaikaribisha Yanga kwenye uwanja wake wa Kambarage ni kuvuna pointi tano katika mechi tatu ilizocheza ikiwa ugenini. Jumapili ligi hiyo iliendelea kwa mchezo mmoja uliopigwa kwenye uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya na wenyeji Tanzania Prisons kufungwa mabao 2-1 na JKT Ruvu ya Dar es Salaaa. Matokeo hayo yamezidi kuidhoofisha Prisons inayofundishwa na kocha David Mwamaja ambaye amemlaumu kipa wake kuwa ndiye aliyeifungisha kutokana na uzembe alioufanya. Na huo umekuwa ushindi wa kwanza kwa kocha wa JKT Ruvu Fred Felix Minziro,ambaye anamwezi wa tano sasa tangu alipoanza kuifundisha timu hiyo baada ya kutimuliwa na klabu ya Yanga alipokuwa kocha msaidizi.
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: