NAPE AWAPONDA UKAWA KWA KUUNGANA, ADAI WAMEJICHIMBIA KABURI WENYEWE
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye amesema hatua ya viongozi wa vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (Ukawa), kuingia katika makubaliano ya kushirikiana “ni kaburi la vyama hivyo.”
Wakati Nape akisema hayo, baadhi ya wasomi wamesema ni hatua kubwa lakini yenye kuhitaji kuwa na sera na itikadi ya pamoja.
Akizungumza kwa simu jana, Nape alisema Ukawa ni kaburi la vyama vya upinzani vilivyoungana kwa kuwa vitapoteza utambulisho wao.
“Huu ni mwanzo wa kumomonyoka kwa vyama vya upinzani, moja vyama hivyo vitapoteza identity (utambulisho) zao na kama mkutano wenyewe ndiyo umehudhuriwa na watu kidogo vile, basi hali yao ni ngumu sana,” alisema Nape.
Alisema kutakuwa na mgogoro mkubwa hasa kwenye nafasi za kugombea kwa kuwa hasa katika majimbo akitolea mfano wa Jimbo la Ubungo ambalo alisema Julius Mtatiro wa CUF anataka kugombea huku John Mnyika wa Chadema naye akitaka kutetea nafasi yake.
“Ukawa ni bomu ambalo litawalipukia na kwangu sijaona jambo jema kwa ushirikiano huo,” alisema Nape.
Hata hivyo, Nape alisema jambo moja ambalo vyama hivyo vimelifanya ni kuunganisha nguvu kupambana na CCM ambayo misuli yake ni mikubwa.
Na Boniface Meena, Mwananchi
0 comments:
Post a Comment