FREEMASONS WAZIDI KULIPASUA KANISA ANGLIKANA

Sakata la baadhi ya waumini wa Kanisa Kuu la Mtakatifu Nicholas Mwanza (DVN) kumkataa Askofu Mkuu, Boniphace Kwangu wakimtuhumu kuwa mwanachama wa imani ya Freemason limechukua sura mpya baada ya baadhi ya waumini juzi (Jumapili) kutotokea kanisani hapo kwa madai kwamba mpaka hali ikae sawa. Baadhi ya waumini hao ambao hawakutaka majina yao yaandikwe, walisema wamepoa majumbani mpaka uongozi utoe tamko linalojulikana la sivyo watahamia makanisa mengine kuliko kusali katika kanisa lenye mgogoro wa kiimani. Hivi karibuni, muumini mmoja wa kanisa hilo, Msoma Lazaro alilazimisha kusoma tamko madhabahuni kwa niaba ya kundi lake akisema Askofu Kwangu haruhusiwi kuendesha ibada kwenye kanisa hilo kuanzia siku hiyo. Hata hivyo, wakati tamko hilo likisomwa na Lazaro, kulizuka vurugu baina ya viongozi wa kanisa hilo na msomaji wa tamko hilo wakizuia lisisomwe kwa madai kuwa ni kuvuruga ibada kwa sababu halikufuata utaratibu. Akiwa katika harakati za kusoma tamko hilo, baadhi ya viongozi walimzuia wakimtaka asubiri kwanza, lakini kutokana na msimamo wake alilisoma tamko hilo kabla ya kuondolewa kwa nguvu na kuporwa karatasi ya tamko hilo ambalo lilikuwa na baadhi ya picha za Askofu Kwangu. Uwazi lilifanikiwa kupata nakala ya tamko hilo la kumkataa Askofu Kwangu likisema kuwa ndiyo mwisho wake wa kutoa huduma zozote za kiroho kanisani hapo na kwingineko kutokana na mambo anayotaka kuyafanya kanisani hapo yenye ishara za kishirikina (Freemason). Waumini waliompinga askofu huyo walisema imethibitika kuwa ameonesha ukweli wa kuondoa zuria (kapeti) ndani ya kanisa kwa sababu za Freemason. Alitaka kuchimbua vigae vya madhabahuni akidai vimejengwa na kuwekwa hirizi na pia ana mpango wa kufukua kaburi la askofu hayati J. O. Rusbamayila aliyezikwa ndani ya kanisa na kulipeleka nje ya kanisa. Baadhi ya waumini wa kanisa hilo walionekana kumtetea Askofu Kwangu kwa kusema kuwa wanaomwandamana ni mashetani wakubwa. Mmoja wa waumini hao, mama Mataba alisema picha zinazomwonesha askofu huyo akiwa na mwanachama wa Freemason ni za kupandikiza na za uongo, kwamba hawezi kujiunga na imani hiyo hata siku moja. “Picha ni za uongo.Tumekuja kusali na kuabudu hatujaja kutoa tamko hilo hapa, hayo mambo yanatoka wapi?” alihoji mama Mataba. Aidha, mmoja wa waumini alisema pete inayovaliwa na askofu huyo haina uhusiano wowote na imani ya Freemason bali baadhi ya waumini wanasema bila kujua pete ya Freemason ikoje. Uwazi lilipozungumza na Askofu Kwangu kuhusu tamko hilo lililosomwa kanisa hapo alisema hajui chochote kwa sababu hakuhudhuria ibada ya siku ya tukio kwa vile alikuwa kwenye sherehe za kusimikwa kwa askofu wa Kanisa la Africa Inland Church Tanzania ‘AICT’ ambaye hakumtaja jina. “Hili tamko limetolewa na nani, maana sijahudhuria kanisani leo. Sisi tulikuwa kwenye ibada ya usimikakwaji wa askofu mwenzetu. Kama limepitia kwenye taratibu zetu halijanifikia. Kama halikupitia katika njia hizo si sawa, ni tamko la barabarani mtu kuota na kutoa tamko,” alisema. Akaongeza: “Naomba nisiwe na Comment katika hilo na naomba usiniulize lolote, sielewi lolote maana sikushirikishwa na sijasali hapo.” Cedit: Uwazi/Gpl
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment

0 comments: