DEREVA TOYO sehemu ya 2
ILIPOISHIA JANA
"mambo?"
"poa tu vp mbona wazazi wako wanagomba au ni mimi nini kuja hapa?"
"aaa wala tu .... hawa wana swaga zao"
"sasa kuna sendof jioni hivyo kama vipi ukapige picha kule gaden rozi"
"ndio huko sendof inakofanyika?"
"ndio"
"ok poa"
"ila usiniangushe na pamba.... maana nikifika pale nitajitangazia kua ni kaka angu"
"haaaa wewe si unanijua milipuko yangu?"
"najua vizuri ila ya leo vunja kabati"
ENDELEAAA....
"kwani vipi kuna shazi ya watu nini?"
Akanijibu "ndio"
nikamuuliza "kutakua na watoto ee?"
Akaanza kununa huku akisema
"ndio maana madili mengi sikupagi"
"aaa reiiii yashakua hayo tena?"
"sasa unaulizia wanawake wa nini?"
"baasi mama eeh?"
Basi tulibembelezana pale mimi na rey... ila rey anaonekana ana chembe chembe za kunipenda.. maana sina uhusiano nae, bali ni jirani yangu tu.a1lqq
Basi nilitoka nae pale na kumpeleka mjini ili akachague viwalo vya sendOf jioni, Tuliingia duka moja livye kuuza nguo za kike tuu.
"sheby hapa hua wanaume tofauti na wapenzi hawaruhusiwagi kuingia"
"haaa kwaio mimi itakuaje? Basi ngoja nitoke nje"
"ah ah bwana usitoke"
"sasa kwani mi ni mpenzi wako?"
"tujifanye tuu"
"acha masihara rey, au kama vp mi nipo nje"
"mmhh sawa kama hutaki"
Basi nilitoka nje huku nikiwa naangaza angaza huku na kule, Maana si unanijua zangu?
Mara Besti yangu kaja na demu wake
"aaahh jemsi vp? afu mbona upo hapa dukani? au umekuja na mtoto nini?"
Aliongea huku akicheka kumaanisha ni utani tu
"wala tu, sema kuna manzi nimemsindikiza saa hii"
"sasa mbona upo nje baba? twenzetu, kwani nami nipo na shemu wako hapa tunachukua viwalo.... Alafu ivi unajua kua jion kuna bonge ya sendof?"
Nikamjibu "ndio nafahamu na ndio maana nimemleta huyo manzi"
Sasa best yangu jackson akaninong'oneza skioni
"we jemsi inamaana kwenye paty hutokua na demu?"
Nikamjibu "mademu nitapata huko huko"
akaniambia
"acha ukiraza wewe, Afu demu mwenyewe si ndio yule?"
Nikamjibu
"ndio yule kwani vp?"
"aaahhh jimiii mbona unaniangusha best?"
"kwanini nakuangusha?"
"ng'oa mtoto yuleee uzame nae patini"
"usijali"
Mara simu yangu iliingia meseji, Nikaifungua na kuisoma, Iliandikwa na rey
"njoo bwana tuchague nguo"
Nikamjibu fasta fasta
"nakuja ila sasa si hadi tuwe wapenzi?"
Akanijibu fasta
"basi nakuruhusu njoo unishike kiuno"
"heeeee tenaa?"
"njoo basi na wewe, si unaona mwenzio kaingia na mpenzi wake?"
Nikajumlisha na yale nilioambiwa na jackson, Niliona ni sawa tu, maana mtoto mwenyewe ni mkali balaa, ila sijui ni kwanini ananikubali hivyo,
Basi niliingia kwa mbwembwe nyingi kisha nikamshika kiuno afu nikamlamba bonge la busu shingoni, maana si nilikua kwa nyuma yake
Na ndio maana nimefanya hivyo, sasa mtoto saa ngapi hajaanza kutulia na kuskilizia lile busu niliompiga..... kisha akageuka na kunitazama huku akijishika shika ile sehemu niliombusu
"jemsi?"
"nini?"
"ivi ni kweli au naota?"
"uoteje sasa?"
"sheby?......fanya kweli basi"
"kweli gani?"
"ngoja tumalize kuchagua nguo nitakuambia"
"mmhh sawa"
Basi tulichagua nguo kwa mbwembwe zote huku mtoto akaniambia tuelekee kwenye nguo za kiume, maana hapo tayari keshachagua na keshalipia mwenyewe, maana rehema kwao sio mbaya saana, Basi tuliagana na rafiki yangu jackson kisha tukatoka na kuelekea kwenye miduka ya nguo za kiume,
"ivi jemsi? Ushawahi kua na mpenzi wewe?"
"ndio tena ninae hadi sasa"
"mmhh ni mzuri ee?"
Mtoto alianza kujishtukia kwa kuhoji miswali isio ya msingi
Sasa rehema anataka kujua kua demu wangu ana uzuri kiasi gani, Na mimi sikumficha nilimpa laivu bila chenga
"ndio ni mzuri, Ana figa, afu mkarimu, pia ni mweupee, afu ananipenda nami nampenda sana"
Mtoto rehema alianza kununa ghafla huku tukikaribia katika duka tuliolikusudia kuingia...
Rehema akaniambia
"hamjawahi kugombana?"
"tuligombana mara moja tu"
"haaa sasa kwanini usimuache?"
"weee nampenda afu ananipenda sana, na ni mwepesi wa kuomba msamaha sana, kwahio nilimsamehe tu"
Rehema Alikosa la kuongea ila tulifika dukani hapo na kuingia kwa mbwembwe nyiingi utafikiri nanunua mimi bwana...
Nikamuuliza rehema "sasa rey? hapa kuna vazi lako kweli?"
Akanijibu kua "hapa nimekuja kwa ajili yako"
Nami nikamuambia "aahh sasa mi sina pesa"
Akanijibu "kwani? umeshachagua nguo na ukaletewa bili ulipe?"
"una maana gani?"
"namaanisha chagua nguo unazopenda hapo na viatu, afu nitalipa"
"acha utani rey"
"kweli vile au nilipe pesa kabisa uone?"
"ok poa ngoja nichague"
Basi mtoto wa kiume niliingia ndani ndani nikavuta pamba za maana na za kisasa zaidi,
Kisha nikavuta TIMSI moja ya maana ( timsi ni viatu fulani hivi vya rangi ya njano au rangi zingine... viatu hivyo vinaitwa TIMBERLAND ila kwa kifupi tunaita TIMSI au AMERIKAN BUTI )
Basi nilivuta viwalo vile huku nikivikagua kwa umakini isijekua mdosho ( spesho )
Basi tulimaliza pale kuchagua moja baada ya nyingine kisha tukatoka pale na kuelekea majumbani kwa ajili ya kujiandaa na sendof ya jion saa kumi,
"rey?"
"mmhh?"
"asante sana, maana najua ninavyo viwalo ila havikutii hivi ulivyo ninunulia"
"usijali bayby"
"nini?"
"
itaendeleaa.....
0 comments:
Post a Comment