LUCY KOMBA AMSHANGAA AUNT EZEKIEL KUISHI MBALI NA MUME…!!


MWANADADA anayefanya poa kwenye
anga la filamu Bongo , Lucy Komba
amejikuta akibaki na viulizo vingi kutokana na kitendo cha msanii mwenzake , Aunt Ezekiel kuishi mbali na mumewe
anayefahamika kwa jina la Demonte kwa
kipindi kirefu, jambo ambalo yeye hawezi kulifanya.
Akizungumza na paparazi wetu , msanii
huyo alisema kitendo cha Aunt kuolewa na
kuishi mbali na mumewe kinamfanya abaki
na maswali mengi kichwani, sababu wanandoa kuishi mbalimbali husababisha
wahusika kuumizana kichwa kwa kiasi kikubwa na kukosa amani ya moyo .
“Namshangaa Aunt anawezaje kuishi,mbali na mumewe kwa kipindi kirefu, binafsi
siwezi. Kama hivi ninavyotarajia kuolewa
hivi karibuni , nimekubali kuachana na dili
zangu zote za hapa Bongo , nikiolewa naenda kuishi Denmark kwa mume wangu ,”
alisema Lucy Komba .

Jivunie kuwa mwana ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment