KILIO HIKI CHA WAKULIMA LUDEWA NANI ATAKIFUTA?

Kilio cha wakulima wadogo wa mahindi Ludewa mkoan Njombe kimezid kusikika kwa nyakati tofaut kufutia mahindi yao kutokidhi viwango vya wakala wa taifa wa chakula NFRA kama Aambavyo ilitanabaishwa na mkuregenzi wa shirika hilo kanda ya makambako ambapo alisema mahind yatakayo chukuliwa ni yale yaliyo safishwa na kuondolewa mahind yote yenye rangi ya njano.
Kila Mtaa wa kata ya Ludewa wakulima hao wanalalamika na shughuli pevu ya kuchambua mahind hayo ili yawe safi ila wamekili kaz hiyo ni ngumu na kamwe haiwez kuwezekana ila chaa ajabu ni pale katika vituo vingine wanavyonunua mahindi hayo yanunuliwa hivyo baadhi ya wakulima wakubwa wanahamisha mahindi yao hadi katika kituo cha mlangali.
Wakulima Hawajui lini mahindi yao yatanunuliwa ambapo mpaka Sasa wafanyakaz hao wana nunua Mahindi kwenye Madebe na Kila Debe ni Shilingi 4000 Tu kwa Debe moja la Mahindi! Huu ni Msiba Mkubwa!Hiki ni Kilio Nani atawafuta Machozi Wakulima Hawa..
Pia mapema wiki hii mkuu wa mkoa wa njombe kap.Msangi alizulu katika maghala ya kununulia chakula ambapo aliwasihi wafanyakaz wa shirika hilo kutenda haki kwa wakulima na kujibu mashtaka kwa nini wamekwenda kinyume na agizo la naibu waziri ambaye naye alifanya ziara wilayan hapa kufuatia mgomo uliotekea siku za mwanzo.
Naibu waziri wa chakula na ushirika Mh.Godifreyi Zambi amelifanya ziara ya kushitukizaa katika ghala la kuifadhia mahindi la ludewa kijijini lilipo wilayani ludewa mkoan njombe kufuatia malalamiko ya wakulima wadogo kutengwa katika ununuzi wa mahindi kutoka kwa wakulima.
Akiongea na wananchi waliokusanyika katika eneo hilo la Ludewa kijijini naibu waziri wa chakula na ushirika mh.zambi amewataka wakala wa taifa wa chakula NFRA kuhakikisha wanatenda haki kwa wakulima wodogo ili kuondoa malalako kwa wakulima hao.
Wananchi hao walitoa malalamiko yako kufutia utaratibu wa kuuza mahindi jinsi ulivyokuwa unaendelea kwa kupima mahindi ya viongoz wa halmashauli na wafanya biashara wakubwa ambao walinunua mahindi kwa wakulima kwa kuwanyonya na wao kuuza kwa wakla wa taifa kwa bei nafuu.
Akijibu tuhuma hizo mkuu wa wilaya wa ludewa Bw.Juma solomon madaha alisema kuwa lawama hizo zinatokana na mfanya biashara mmoja kupima magunia 1500 ya mahindi .
Pia naibu wazir ameongeza kuwa ni vyema kuanza kupima mahindi ya wakulima wadogo ambao wana magunia yasiyozidi 50 baada ya hapo waje wakulima wakati na kisha wakubwa pamoja na wafanya biashara..
Tangu siku ya jumanne mahindi katika kata ya ludewa kijijini yalikuwa hayapimwi hali ambayo inazid kuleta wasiwasi kwa wakulima hao na wengine wakisisitiza kugomea kupiga kura katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa na uchaguz mkuu.
Kilio hiki cha wakulima nan atakifuta...

Jivunie kuwa mwana ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment