ZOEZI LA UORODHESHAJI WA VIWANDA WILAYA YA LUDEWA LIMEANZA RASMI

Ludewa
Na barnabas njenjema

Wito umetolewa kwa wamiliki wote wa viwanda waliopo katika wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe kutoa taarifa sahihi na ushirikiano wa kutosha kwa wadadisi wakaopita katika viwanda vyao ili kufanya zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda kwa ajili ya maandalizi ya Sensa ya Viwanda inayotarajia kufanyika mwezi Septemba, 2014.
Akizungumza na waandishi wa habari leo mkoani Iringa, kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu, Meneja Takwimu mkoa wa Iringa na Njombe Fabian Fundi amesema zoezi hilo linaanza rasmi leo tarehe 25 Agosti, 2014 na litamalizika siku ya Jumapili tarehe 31 Agosti, 2014.
“Zoezi la Uorodheshaji wa Viwanda wilaya ya Ludewa linaanza rasmi leo na litahusisha jumla ya kata kumi na sita ambazo ni pamoja na Ludende, Lugarawa, Ruhuhu, Lupanga, Lwela, Mavanga na Mundindi”, amesema Fundi.
Amezitaja kata nyingine kuwa ni, Ibumi, Mlangali, Kilondo, Madope, Lupingu, madilu, Makonde, Mkongobaki na Lifuma.
Fundi amefafanua kuwa taarifa zinazokusanywa katika zoezi hili kutoka viwandani ni pamoja na jina la kiwanda, anuani za kiwanda, mahali kiwanda kilipo, aina ya umiliki na utaifa wa mmiliki.
Taarifa nyingine ni gharama za malipo mbalimbali kwa wafanyakazi, mwaka kiwanda kilipoanzishwa, aina ya bidhaa zinazozalishwa, idadi ya wafanyakazi na gharama za uzalishaji.
Zoezi hili la Uorodheshaji wa Viwanda lilianza tarehe 8 Aprili, 2014 kwa Tanzania Bara na mpaka sasa karibu maeneo yote zoezi hili limekwisha kamilika.
Jivunie kuwa mwana ludewa
Share on Google Plus

About Rafiki Fm Ludewa

This is a short description in the author block about the author. You edit it by entering text in the "Biographical Info" field in the user admin panel.
    Blogger Comment
    Facebook Comment