JUHUDI ZAFANYIKA KUWATOMEZA SIMBA WALIOVAMIA MAKAZI YA YATU WILAYANI LUDEWA
Ludewa
Na.barnabas njenjema
Kamati ya ulinzi na usalama Wilayani Ludewa Mkoani Njombe chini ya mwenyekitiki wake ambaye pia ni mkuu wa Wilaya ya Ludewa Juma Solomon Madaha amewataka wananchi wote wilayan hapa kuwa na umoja na kutoa taarifa pindi simba hao watakapooneka.
Ikumbukwe kuwa wiki iliyopita simba wawili waliingia wilayani hapa na sasa imebainika kuwa wapo watatu walivamia maeneo ya ngelenge katika kijiji cha manda na kuleta madhara kwa wananchi kwa kula mifugo yao.
Kwa sasa simba hao wamezid kusogea mbele zaid inaripotiwa kuwa wapo kati ya kijiji cha nkomang'ombe na milo wilayan ludewa.
Akizungumza na waandishi wa habari ofisin kwake mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya ludewa alisema amepata taarifa kupitia mitandao lakin baadae alipewa taarifa na diwan wa kata husika ndipo hatua mbali mbali zimeanza kuchukuliwa.
Akizitaja hatua izo zilizochukuliwa mpaka sasa ni pamoja na kutoa taarika game reselve ambao kwa mkoa wa Njombe wanapatika katika halmashauli ya mji wa Njombe ambapo wameshatuma gari kwenda kuwachukua wataalam hao ili waje kuwaangamiza simba hao wanaozid kuleta madhala makubwa kwa wananchi."sisi tunawajibu wa kuwalinda raia na mali zao hivyo bhas tutahakikisha wananhi wanakuwa katika hali ya aman muda wote"aliongeza bw.Madaha.
Hata ivyo kwa upande wake hakusita kutoa pole kwa wananchi wote walipatwa na majanga ya kuuliwa kwa mifugo yao na wananchi wote walidhulika kwa namna moja ama nyingi.
Kwa upande wa wananchi waliopatwa na majanga hayo wanaiomba serikali kafanya haraka zaid kuhakikisha simba hao wanauliwa mapema ili wasizid kuleta maafa zaid kwa wananchi,,
"tunaiomba serikali ifanye haraka zaid kwa hata sisi tumejawa na hofu hatutembei wala kufanya shughuli za maendeleo kutokana na simba waliopo hapa kijijin."alisema mmoja wa wanakijiji wa kijiji cha ngelenge.
Simba hao waliingia wilayan ludewa kutokea katika wilaya ya nyasa iliyopo mkoani ruvuma.
Jivunie kuwa mwana ludewa
Blogger Comment
Facebook Comment